1.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akisikiliza hoja ya mjumbe
(hayupo pichani) wa kikao kuhusu namna bora zaidi ya uwekezaji katika
sekta ya mifugo kutokana na nia ya serikali ya Misri kutaka kuwekeza
katika sekta hiyo.
2.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akisoma baadhi ya
mapendekezo yaliyoandaliwa na wajumbe wa kikao (hawapo pichani), kuhusu
uwekezaji katika sekta ya mifugo kutokana na nia ya serikali ya Misri
kutaka kuwekeza katika sekta hiyo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.
Luhaga Mpina akifafanua jambo kwa wajumbe wa kikao (hawapo pichani) njia
bora zaidi za uwekezaji katika sekta ya mifugo kutokana na nia ya
serikali ya nchi ya Misri kutaka kuwekeza katika sekta hiyo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.
Luhaga Mpina akisikiliza hoja mbalimbali za wajumbe kuhusu uwekezaji
katika sekta ya mifugo, kutokana na nia iliyooneshwa ya uwekezaji na
serikali ya Misri.
…………………
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.
Luhaga Mpina ameongoza kikao cha wakuu wa idara zilizo chini ya wizara
yake pamoja na wadau wengine wa sekta ya mifugo, kujadili namna bora
zaidi ya serikali ya Tanzania inavyoweza kunufaika na uwekezaji katika
sekta ya mifugo kutokana
na nia ya serikali ya Misri kutaka kuwekeza
katika sekta hiyo iliyooneshwa katika siku chache zilizopita.
Akizungumza katika kikao hicho
kilichofanyika ofisi ndogo za wizara hiyo Jijini Dar es Salaam, Mhe.
Waziri Mpina amewaambia wajumbe wa kikao hicho wakiwemo wawakilishi
kutoka SUMA JKT, Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) na Dawati la Sekta
Binafsi, kuwa na mikakati ambayo itasaidia uwekezaji huo uwe na tija kwa
taifa.
Aidha Waziri Mpina amesema
serikali inahitaji wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi, lakini ni
muhimu yakaandaliwa mazingira bora zaidi ili uwekezaji huo uwe endelevu
na kuleta tija kwa taifa na wananchi kwa ujumla.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria
kikao hicho, wamemshauri Mhe. Waziri Mpina masuala mbalimbali yakiwemo
ya kitaalam pamoja na vifungu vya kisheria ili mikataba itakapoandaliwa
na kusainiwa kati ya serikali ya Tanzania na Misri iweze kuleta faida
kwa nchi hizo mbili.
Hivi karibuni Kaimu Balozi wa
Misri nchini Bibi. Neville El-Saeed na Mkuu wa kitengo cha Uchumi katika
ubalozi huo Bw. Mohamed Ibrahim, walifika katika ofisi ndogo za wizara
hiyo katika siku tofauti tofauti ambapo walipata fursa ya kuzungumza na
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina kuhusu uwekezaji huo.
Maafisa hao pia walikutana na
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia (Mifugo) Prof.
Elisante Ole Gabriel na kumkabidhi andiko la awali la nia ya serikali ya
nchi hiyo kutaka kuwekeza katika sekta ya mifugo na kufungua fursa
zaidi zilizopo katika sekta hiyo.
No comments :
Post a Comment