Meneja Kiongozi Mkuu wa Masoko na Uhusiano
wa PSSSF, Eunice Chiume. Picha ya maktaba yetu.
Na Christian Gaya: Ijumaa, 2 Novemba 2018: www.majira.co.tz
KATIKA mkakati wa kuboresha huduma na kupunguza
matumizi katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini, Serikali iliamua kuunganisha
Mifuko minne ya PSPF, PPF, GEPF na LAPF na kuunda Mfuko mmoja
unaojulikana kama Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa ...
Umma
(PSSSF).
Aidha ili kuhakikisha huduma
hizo zinatolewa kwa ufanisi zaidi na kurahisisha utekelezaji wa Sheria ya
Hifadhi ya Jamii, Serikali pia iliamua Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii NSSF
uendelee na jukumu la kuhudumia wafanyakazi wa Sekta Binafsi na Sekta Isiyo
rasmi tu.
Hivyo
basi, Meneja Kiongozi Mkuu wa Uhusiano na Masoko wa mfuko wa PSSSF Eunice Chiume, anasema wanachama wote ikiwa
ni pamoja na wastaafu na warithi waliopo katika mifuko inayounganishwa tayari wamehamishiwa
katika mfuko wa PSSSF na haki na stahili zao sasa zinaendelea kutolewa na mfuko
huo.
“Hii imejumuishwa
pamoja na rasilimali, vitega uchumi, madeni, mifuko ya hiari na mikataba
iliyokuwa chini ya mifuko inayounganishwa nayo tayari imeshahamishiwa kwenye
mfuko huu mpya wa PSSSF” Chiume anaongezea.
Anasema baada ya
kutangazwa kuanza kwa Mfuko wa PSSSF, pamoja na mambo mengine uongozi mpya ulikuwa
na jukumu la kwanza la kulipa madeni ya malipo ya mkupuo kwa wanachama wa waliokuwa
wa mfuko wa pensheni wa PSPF.
Chiume anasema idadi
yao ilikuwa ni wastaafu wapatao 7,924 wenye jumla ya Sh. bilioni 738.43 za
Kitanzania. Na mpango huu wa kulipa madeni haya uliidhinishwa na Bodi ya PSSSF kwa
kuzingatia mtiririko wa kifedha kwa kipindi cha miezi 6 kuanzia Agosti 2018.
Anasema kwa Agosti 2018
tu Mfuko wa PSSSF uliwalipa wastaafu wapatao
896 hawa wakiwa ni wa Julai 2017 tu, ambapo kati hao 755 wakiwa wa fao la
kustaafu na wapatao 141 wakiwa wanufaika wa fao la urithi na hivyo basi Mfuko
ulitumia jumla ya Sh.65,381,743,855.48 kwa wastaafu wote. Hii ikiwa ni mara tu Serikali ilipotangaza rasmi kuanza kutumika kwa Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii kwa Watumsihi wa Umma (PSSSF) Agosti1.
“Orodha iliyohakikiwa
na Hazina na kupitishwa kwa ajili ya malipo ina wastaafu wa umri wapatao 5,904.
Kati ya hao hundi zipatazo 1,123 zenye jumla ya Sh. 94,484,375,322.57 zikiwa ni
zile zilizotakiwa kulipwa kati ya mwezi Agosti mpaka Novemba 2017 zilitolewa kwa
malipo kati ya Oktoba 5 na Oktoba mwaka huu.
Ambapo kati ya Wastaafu wapatao 814 wa mwezi Desemba 2017 wanategemewa
kulipwa mwishoni mwezi huu wa Oktoba 2018,” Chiume anafafanua.
Anasema kwa Novemba
2018 watalipwa wastaafu wapatao 1,603 hawa wakiwa ni wale wa mwezi Januari –
Machi 2018. Wakati kwa Disemba 2018 wamepagwa kulipwa wastaafu 931, wakati wa
Aprili - Mei 2018 na waliobaki 1,372 watalipwa Januari 2019.
Anasema wastaafu wapatao
1,292, Hazina ilishauri wafanyiwe kwanza uhakiki zaidi kabla ya kuanza kulipwa pensheni
zao, ambapo kati yao wapo waliondoka kazini kwa kufukuzwa, kuacha kazi, kuwa na
umri zaidi ya miaka 60, vyeti feki na marekebisho ya muundo.
Malipo ya wastaafu walioingia
kwenye Mfuko mpya wa PSSSF kuanzia tarehe mosi Agosti 2018 na kuendelea, wao wanaendelea
kulipwa, ambapo hadi sasa madai yapatayo 326 yameshalipwa tayari. “Lengo Letu ni
kuendelea kuwalipa ndani ya muda unaotajwa kisheria hadi madai ya nyuma
yatakapokamilika na baada ya hapo watalipwa mapema zaidi.” Alifafanua zaidi.
Anasema wakati madai ya
kipindi kabla ya kuanza kwa Mfuko wa PSSSF ambayo hayakuwa yamelipwa na mifuko kutokana
na sababu mbalimbali yameletwa makao makuu kwa ajili ya kukamilishwa na
kuandaliwa malipo. Madai hayo ni jumla
ya 3,876 yakijumuisha madai ya mafao ya uzazi, malipo ya mfumo wa hiari,
kujitoa na kupunguzwa kazi. “Madai hayo sasa yameletwa hapa PSSSF makao makuu Dodoma
kwa uchambuzi na malipo kwa madai yanayostahili,” Chiume anaeleza
Wakati huo huo, Chiume anasema mifumo
mikuu mitatu ya kielektoniki tayari imeshaandaliwa na iko katika hatua za
mafunzo kwa watumiaji mikoani baada ya kuwa imehakikiwa makao makuu.
“Mifumo hii ni mfumo wa
kutunza kumbukumbu za wanachama yaani SSIP, mfumo wa mishahara ya watumishi na
mfumo wa fedha yaani Navision Dynamics.
Mifumo mingine kama vile barua pepe za watumishi wa Mfuko na tovuti, iko
tayari. Tovuti itakuwa hewani muda si mrefu baada ya kuwekewa taarifa zote muhimu.
Anafafanua ya kuwa
ofisi zimefunguliwa nchi nzima na tayari watumishi wamehamishiwa. Kazi
inayoendelea kufanyika ni kuunganisha mifumo iliyotajwa hapo kwenye ofisi hizo
kuhamisha samani na vitendea kazi pamoja na kuzifanyia kuwekewa alama za Mfuko wa
PSSSF yaani branding.
Kwa upande wa uhamisho
wa watumishi, anasema tayari watumishi wa Mifuko yote yaani wa kutoka LAPF,
PPF, PSPF, na GEPF wamesha pangiwa vituo na kuhama, tayari kwa ajili ya kutoa
huduma vituoni mwao.
Wakati kwa upande wa
kufunga hesabu za mifuko, Eunice anaeleza ya kuwa hesabu za mifuko iliyoungana
zimeshafungwa na sasa kazi ya ukaguzi inakamilishwa tayari. “Hesabu hizo
zitajumuishwa kuwa hesabu za mwanzo za Mfuko wa PSSSF. Kazi hii ya kuunganisha
inategemewa kukamilika mwezi Desemba 2018,” Chiume anafafanua zaidi.
Kwa upande wa taarifa
kwa waajiri, anasema waajiri wanaendelea kutembelewa na kupewa taarifa juu ya
kuunganishwa kwa mifuko na utaratibu wa kuwasilisha michango. Pamoja na haya
yote, hata akaunti mpya za mfuko zimeshafunguliwa tayari kila mkoa kwa ajili ya
kupokelea michango kutoka kwa waajiri wote nchini.
No comments :
Post a Comment