Waziri
wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) akitoa maelekezo katika kizimba cha kupunguza msukumo wa maji
(BPT) katika eneo la mto Simba, wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro. Mradi wa
maji wa Longido chanzo chake kipo mkoani Kilimanjaro.
Waziri
wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa akiangalia ubora wa kizimba na bomba zilizotumika katika kizimba cha
kupunguza msukumo wa maji (BTP) katika eneo la mashamba la Simba. BTP moja ya
kazi yake ni kuzuia mabomba kupasuka. Mradi wa maji wa Longido mabomba
yamelazwa kwa umbali wa kilomita 94 na thamani ya mradi ni kiasi cha Shilingi
bilioni 15.7.
Waziri
wa Maji Profesa Makame Mbarawa (Mb) akishiriki kazi ya kuunga mabomba kabla ya kulazwa eneo la Mbugani, katika
mradi wa maji wa Longido . Waziri Mbarawa amemtaka mkandarasi kampuni ya Ujenzi
ya STC kukabidhi mradi ifikapo Tarehe 15 Desemba 2018.
No comments :
Post a Comment