Friday, November 2, 2018

NAIBU SPIKA ATEMBELEA MAONESHO YA WIKI YA VIWANDA PWANI


V2
NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji kiuchumi mkoa wa Pwani, Jovita Noah, wakati alipotembelea Banda la Wajasiriamali hao katika maonesho ya Wiki ya Viwanda yanayoendelea katika Uwanja wa Sabasaba Picha ya Ndege Kibaha, juzi (jana).
V4
NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson, akivishwa vazi la asili na kama zawadi aliyopewa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji kiuchumi mkoa wa Pwani, Jovita Noah, wakati alipotembelea Banda la Wajasiriamali hao katika maonesho ya Wiki ya Viwanda yanayoendelea katika Uwanja wa Sabasaba Picha ya Ndege Kibaha, juzi ( jana).
V5
NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha kuzalizsha nguzo za umeme za zege cha East Africa Infrastructure Engineering Ltd, Johnspeter Majura, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya Maonesho ya wiki ya Viwanda, kwenye Uwanja wa Sabasa Pichaya Ndege Kibaha, mkoa wa Pwani juzi. Kushotokwake ni Mkuuwa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo
V6
NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mdhibitishaji ubora wa Kampuni ya Elven AgriCo. Ltd, Gilbert Kimaro, kuhusu matunda yaliyokaushwa wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye maonesho ya wiki ya Viwanda kwenye Uwanja wa Sabasa Picha ya Ndege, Kibaha mkoa wa Pwani juzi (jana). Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, akikagua bidhaa hiyo. Kulia ni mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumta Mshana.
V7
NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Masoko wa Kiwanda cha kusindika Samaki cha Alpha Krust, Joyce  Mrutu, wakati akiangalia pakiti iliyojazwa samaki alipokuwa akitembelea mabanda kwenye maonesho ya wiki ya Viwanda uwanja wa Sabasaba Picha ya Ndege Mkoa wa Pwani, juzi (jana).
Picha na Muhidin Sufiani)

No comments :

Post a Comment