Balozi wa Korea Kusini, Mh. Geum
Young Song (katikati) akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Elimu katika
Shirika la UNESCO, Faith Shayo (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye
hafla ya uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika
katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi
wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika. Kushoto ni
Afisa Utawala Msaidizi na Itifaki wa ofisi za Unesco Dar es Salaam,
Rahma Islem.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu katika
Shirika la UNESCO nchini, Faith Shayo akitoa neno la ukaribisho wakati
wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika
hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye
lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
Kutoka kushoto ni Mratibu wa mradi
wa BEAR ll, kutoka makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la
Sayansi Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Whan Sik Kim, Katibu Mtendaji wa
Tume ya Taifa ya Unesco, Dr. Hamisi Malebo, Mkurugenzi wa Elimu ya
Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu Sayansi na
Teknolojia, Dk. Noel Mbonde, Balozi wa Korea Kusini, Mh. Geum Young Song
pamoja na Mratibu wa mradi wa BEAR II kutoka ofisi za Unesco Nairobi,
Bw.Teeluck Bhuwanee wakiwa meza kuu wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR
ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard
jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora
kwa mataifa ya Afrika.
Mratibu wa mradi wa BEAR II kutoka
ofisi za Unesco Nairobi, Bw.Teeluck Bhuwanee akizungumza kwa niaba ya
Mkurugenzi wa UNESCO ukanda wa Afrika Mashariki, Anne Therese Ndong
Jatta Kusini wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya
kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es
Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya
Afrika.
Balozi wa Korea Kusini, Mh. Geum
Young Song akitoa salamu za serikali ya Korea Kusini wakati wa uzinduzi
wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya
Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la
kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na
Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk.
Noel Mbonde akizungumza kwa niaba Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Leonard
Akwilapo wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi
uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR
ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
Mratibu wa mradi wa BEAR ll,
kutoka makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na
Utamaduni (UNESCO) Bw. Whan Sik Kim, akiwasilisha mkakati wa taasisi
hiyo kuhusu ufundi stadi na maana yake katika mradi wa Bear ll nchini
Tanzania wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi
uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Wasilisho hilo lilikuwa ni pamoja na matokeo ya utafiti.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa
ya Unesco, Dr. Hamisi Malebo akitoa neno la shukrani kwa serikali ya
Korea ya Kusini kupitia Shirika la KOICA kwa ufadhili wakati wa uzinduzi
wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya
Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la
kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
Injinia Enock Kayani kutoka Wizara
ya Elimu Sayansi na Teknolojia akizungumzia mradi na matokeo yake
wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika
katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni
mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
Mkurugenzi Mtendaji Mamalaka ya
Mafunzo ya Amali visiwani Zanzibar, Bw. Bakari Silima akitoa wasilisho
kuhusu mradi unavyoweza kutekelezwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR
ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard
jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora
kwa mataifa ya Afrika.
Pichani juu na chini ni sehemu ya
wadau kutoka MoEST, Wizara wa Kilimo, UNESCO, NACTE, TCCA, ATE, VETA
pamoja wadau wa maendeleo walioshiriki uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na
warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini
Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa
mataifa ya Afrika.
Pichani juu na chini ni washiriki
kutoka MoEST, Wizara wa Kilimo, UNESCO, NACTE, TCCA, ATE, VETA pamoja
wadau wa maendeleo wakijadili mwongozo kuhusu makubaliano ya utekelezaji
wa mradi wa BEAR II kwenye vikundi kazi wakati wa uzinduzi wa mradi wa
BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea
Courtyard jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja. BEAR ll ni
mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
Mgeni rasmi pamoja na washiriki wa
uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika
hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya
pamoja. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya
Afrika.
………………………
Na Mwandishi wetu
MRADI mkubwa wa kufunza walimu wa
wasimamizi wa mafunzo ya ufundi standi umezinduliwa kwa kufanyika kwa
warsha itakayosaidia kutoa mwelekeo wa mradi .
Akizungumza katika warsha ya mradi
huo wa BEAR ll unaofanyika katika nchi tano zikiwamo
Tanzania na Uganda
katika awamu yake ya pili, Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya
Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk Noel Mbonde
akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Leonard Akwilapo alishukuru
serikali ya Korea na UNESCO kwa kusaidia kupatikana kwa elimu hiyo
nchini.
Nchi zingine ni Ethiopia, Kenya, Madagascar, Tanzania na Uganda.
Alisema elimu hiyo itasaidia kuboresha na kuleta uwiano kati ya mafunzo ya ufundi stadi na matumizi yake katika viwanda nchini.
Alisema kuna malalamiko kwamba
wahitimu wanashindwa kwenda sanjari na matakwa ya shughuli zao katika
viwanda hivyo mradi huo ni msaada mkubwa.
Mradi huo wenye changio la dola za
Marekani milioni 1.56 kwa kipindi cha miaka mitatu zinatarajiwa
kusambazwa kwa mamlaka mbalimbali za mafunzo nchini yakiwemo mafunzo ya
ufundi stadi zitakazowezesha wafundishaji kutoa mwanga unaotakiwa kwa
mafundi stadi. Mamlaka hizo ni pamoja na TCU, Baraza la Ithibati (NACTE)
nakadhalika.
Alisema mradi huo anaamini utatafuta tatizo la kutoa mafunzo kwa walimu wa ufundi na kuoanisha mahitaji ya viwanda.
Alisema ingawa awamu ya kwanza
haikufika nchini Tanzania, awamu hii ya pili iliyoletwa nchini kwa miaka
mitatu ina msaada mkubwa kwa watanzania ambao wanajiandaa kuwa nchi ya
viwanda.
Pamoja na kushukuriwa, Balozi wa
Korea Kusini, Mh. Geum Young Song amesema taifa lake litaendelea
kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha kwamba linawezesha
elimu ambayo ni msingi mkubwa wa maendeleo.
Alisema kwamba nchi yake ipo tayari kusaidia Tanzania katika elimu na kilimo kupitia Shirika lake la KOICA.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Elimu
katika Shirika la UNESCO, Faith Shayo alisema kwamba lengo kubwa la
mradi huo ni kuboresha mafunzo ya ufundi nchini.
Pamoja na maboresho pia lengo
lilikuwa kuweka njia inayouwiana na masomo hayo ili kuhakikisha kwamba
yanachangia katika ukuaji wa uchumi wa viwanda nchini.
Mratibu wa mradi wa BEAR II,
Bw.Teeluck Bhuwanee alisema ni matumaini yake kwamba ushirikiano kati ya
serikali, Korea Kusini na Unesco utasaidia kuboresha elimu ya ufundi
nchini.
Kuzinduliwa kwa BEAR II
kunaashiria utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa kuendeleza utaalamu
(NSDS) kuanzia mwaka 2016/17 hadi 2025/26 wenye lengo la kuwa na
wafanyakazi wataalamu na wenye ushindani.
Katika warsha hiyo Wizara ya Elimu
Sayansi na Elimu ya Juu imesema kwamba itahakikisha kuwa mradi huo
unafanikiwa na kuwataka wadau wote kushiriki katika kuufanikisha .
Aliwataka kila mdau kuikumbatia dira mpya ya utendaji inayobuniwa na kufikiriwa katika Bear ll kwa lengo la kuimarisha uchumi.
Bw. Teeluck Bhuwanee, akizungumza
kwa niaba ya Mkurugenzi wa UNESCO ukanda wa Afrika Mashariki, Anne
Therese Ndong Jatta, alisema kwamba kuna kazi kubwa inayotakiwa kufanywa
ili kuvikokoa viwanda.
No comments :
Post a Comment