Friday, November 16, 2018

MEYA WA CHADEMA MANISPAA YA IRINGA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA


MEYA ALEX KIMBE AKIFIKISHWA MAHAKAMANI NA MAOFISA WA TAKUKURU LEO
Na Francis Godwin,Iringa
TAASISI  ya  kuzuia na kupambana na Rushwa  nchini (TAKUKURU) imemfikisha   mahakamani mstakihi   meya  wa  halmashauri ya  manispaa ya  Iringa Alex  Kimbe kupitia  chama  cha  demokrasia na maendeleo ( CHADEMA)   makosa  mawili  ya  jinai kuomba na  kupokea  rushwa .
Kaimu  kamanda  wa  takukuru  mkoa  wa  Iringa  Mweli Kilimali   akizungumza leo na  vyombo  vya habari  ofisibni  kwake  alisema kuwa   meya  huyo alipokea kiasi cha  shilingi  milioni 2  kutoka kwa  mteja  wao .
Alisema  kuwa  tukio  la kukamatwa meya  huyo lilitokea  Novemba  15  mwaka  huu majira ya
saa 12  jioni  katika  Hotel ya  Gentle Hills mjini  Iringa .
Kuwa meya  huyo  ambae ni diwani wa kata  ya  Isakalilo  aliokea  pesa   hizo  kinyume na kifungu  cha  15 (1) (a) cha sheria  ya kuzuia na  kupambana na rushwa namba 11/2007.
Alisema  meya  Kimbe  alipokea fedha  hizo za mtego  wa rushwa   akiwa  kwenye gari yake  aina ya  nadia yenye  rangi ya Marron ikiwa na namba  za  usajili T 456 CKD iliyokuwa  imeegeshwa  katika  eneo la  kuegesha magari kwenye  hoteli  hiyo .
“ Maafisa wa  takukuru waliweza kumfuatilia  meya huyo kwa  muda mrefu  na hivyo  kuweza  kumkamata akiwa  amekwisha pokea  fedha  hizo  za  mtego kutoka kwa  mtoa taarifa  wao “
Kilimali  alisema  kuwa  awali  walipokea  taarifa  ya  kuwepo  kwa  ushawishi  wa  kutoka kwa meya huyo kwenda kwa mmoja kati ya  wakandarasi wanaoendesha  tenda  katika Manispaa ya  Iringa ili  muda ukiisha  apate nafasi ya  kupata  tenda  husika .
Hivyo meya  huyo  alimuomba mtoa  taarifa  rushwa na shilingi  milioni 10  na baada  ya  mtoa taarifa  kujitetea hatokuwa na uwezo wa  kutoa fedha hizo mtuhumiwa alikubali  kupokea shilingi milioni 2.
Akiwa  mahakamani  Mwendesha mashtaka   upande  wa  jamhuri  Restuta  Samson  alisema  hamakamani hapo  jana    kuwa    Kimbe  anashitakiwa  makosa  hayo mawili  likiwemo la  kuomba  rushwa  ya  shilingi milioni 10 kutoka kwa Nance  Nyalusi  kama  zawadi baada ya  kupata  zabuni ya kukusanya  ushuru stendi kuu ya mabasi  mjini  Iringa .
Kuwa  mshitakiwa  alifanya  kosa  hilo  kinyume na  sheria  kwa meya  kuomba  zawadi  hiyo  kutoka kwa  mzabuni  huyo .
Wakati  shitaka la  pili  ni   mshitakiwa  amefikishwa  mahakamani hapo kwa  kosa la  kupokea  rushwa  kutoka  kwa  Nance  Nyalusi .
Hata hivyo   mshitakiwa  huyo  aliweza  kukana makosa  yote  yanayomkabili  kuwa  si ya kweli  na  kwa  kuwa upande wa  wakili  wa jamhuri katika  kesi  hiyo  uliieleza mahakama  hiyo kuwa  upelelezi  bado  haujakamilika   na hauna  pingamizi  juu ya  dhamana ya  mshitakiwa .
Hakimu wa  mahakama   hiyo Liad Chamshana  alisema  hamaka  yake  inamtaka  mshitakiwa  kusaini   dhamana ya maadishi ya  shilingi  milioni 10 pamoja na  kuwa  na wadhamini  wawili  mashariti  ambayo  yalitekelezwa na  mshitakiwa  kuachiwa  kwa  dhamana .
Akizungumza nje ya  mahakama  na  waandishi wa habari wakili anayemtetea  Kimbe   Lutebuka  Samson Antony  alisema  kuwa kosa  la  kwanza  linalomkabili mtaja wake ni  kudhaniwa  kuomba  rushwa  huku  kosa la  pili ni la kudhaniwa  kupokea  rushwa  kesi  hiyo  itatajwa  tena  Desemba 5 mwaka huu  .

No comments :

Post a Comment