Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Kangi Lugola akiingia Kituo cha Polisi Tabata, jijini Dar es Salaam
alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha polisi hicho kwa lengo
la kuboresha utendaji kazi wa Jeshi la Polisi nchini. Pia Lugola
alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha polisi Buguruni jijini
humo leo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Kangi Lugola akiwaita majina watuhumiwa (hawapo pichani) waliopo katika
mahabusu ya Kituo cha Polisi cha Tabata, jijini Dar es Salaam, leo, ili
kujua aina ya makosa waliotuhumiwa pamoja na kujua muda waliokaa katika
kituo hicho endapo imefika zaidi ya saa 24 bila kupewa dhamana. Pia
Lugola alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha polisi Buguruni
jijini humo leo. Lengo la ziara hiyo ni kuboresha utendaji kazi wa Jeshi
la Polisi nchini
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Kangi Lugola (kulia) akimuhoji Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Tabata,
jijini Dar es Salaam, Bakari Gothi (watatu kushoto) kuhusu masuala
mbalimbali ya utendaji kazi katika kituo chake, mara baada ya Waziri
huyo kufanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho leo. Pia Lugola
alifanya ziara kama hiyo katika Kituo cha Polisi Buguruni jijini humo.
Lugola anafanya ziara ya kushtukiza katika vituo mbalimbali nchini kwa
lengo la kuboresha utendaji kazi wa Jeshi la Polisi nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Kangi Lugola (katikati) akionyeshwa taarifa za watuhumiwa waliopo
mahabusu ya Kituo cha Polisi cha Buguruni, jijini Dar es Salaam, leo,
wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo hicho kwa
lengo la kufuatilia utendaji kazi. Pia Lugola katika siku hiyo hiyo
alifanya ziara ya aina hiyo katika kituo cha polisi Tabata, jijini humo.
Kulia ni Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kipolisi Buguruni, Adam Maro.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Kangi Lugola (katikati) akimpa maelekezo Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Ilala, Salum Hamduni, mara baada ya Waziri huyo kumaliza ziara yake ya
kushtukiza katika Kituo cha Polisi cha Tabata na Buguruni jijini Dar es
Salaam, leo. Lugola alisema lengo la ziara hiyo ni kuboresha utendaji
kazi wa Jeshi la Polisi nchini. Kushoto ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya
Kipolisi ya Buguruni, Adam Maro.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
………………
Na Felix Mwagara, MOHA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Kangi Lugola, amefanya ziara ya kushtukiza kituo cha Polisi Tabata na
Buguruni vya jijini Dar es Salaam ili kujua
kama maagizo yake aliyoyatoa
katika vituo mbalimbali kama yameanza kufanyiwa kazi.
Waziri Lugola alianza ziara yake
saa 2:45 asubuhi kwa kuibukia katika kituo cha Tabata na moja kwa moja
alianza kuulizia mahudhurio ya wafanyakazi wote wa kituo hicho na kujua
nani yupo kazini na nani hayupo na kwanini hajafika ofisini hapo kwa
muda huo wa asubuhi.
Wakati alipokua kituoni hapo, pia
Lugola alikichukua kitabu cha taarifa za watuhumiwa wote waliopo
mahabusu na baadaye kuelekea katika mahabusu hiyo akiwahoji watuhumiwa
kwa kuwaita kwa majina kujua makosa yao yaliyoyafanya wawepo kituoni
hapo.
Lugola baada ya kumaliza katika
kituo hicho, saa 5:27 alielekea kimyakimya katika kituo cha Polisi cha
Buguruni, na aliwahoji watuhumiwa waliopo mahabusu katika kituo hicho na
kujua makosa mbalimbali yanayowakabili huku polisi wapepelezi wa tuhuma
zao wakiwepo katika tukio hilo.
Akizungumza mara baada ya kumaliza
ziara yake, Lugola alisema, alitoa maagizo mbalimbali katika ziara zake
nchini, hivyo anafuatilia kujua maagizo yake yameanza kufanyiwa kazi au
bado baadhi ya vituo kama wameyapuuza.
“Lengo la hii ziara yangu ni
kuboresha utendaji kazi wa vituo vya polisi nchini, sijaja kumuadhibu
mtu mimi, hivyo msiwe na wasiwasi, bali kilichonifanya hapa nije
nikufuatilia maagizo mbalimbali ambayo niliyatoa kama kweli mnayafanyia
kazi,” alisema Lugola.
Maagizo aliyoyatoa mwezi miwili
iliyopita katika ziara zake mikoa mbalimbali nchini ni kuhakikisha
pikipiki zinaondolewa katika vituo vya polisi, dhamana zitolewe saa 24
ikiwemo Jumamosi na Jumapili, pamoja na polisi kutowabambikizia kesi
wananchi.
Hata hivyo, Lugola alivipongeza
vituo hivyo vya polisi vilivyopo wilayani Ilala na pia Kituo Kikuu cha
Polisi Dodoma alichokitembelea wiki iliyopita, kwa kuanza kuyafanyia
kazi maagizo yake aliyoyatoa zikiwemo baadhi ya bodaboda, zimeondolewa
vituoni na zilizobaki zina kesi mahakamani.
“Nilifanya ziara ya kushtukiza
pale Kituo cha Polisi cha Tabata, na pia nimekuja hapa Buguruni,
kwakweli wameaanza kuyafanyia kazi maagizo yangu, pikipiki zote
nilizozikuta zinasababu yakuwepo hapo, na si vinginevyo kama walivyokua
wanaziweka kiholela hapo awali,” alisema Lugola.
Pia lugola aliwataka Makamanda wa
polisi nchini kuwafuatilia askari wao kwa umakini ili kujua utendaji
kazi wao, na pia Waziri huyo alisema atakua anafanya ziara kama hizo
mara kwa mara hivyo vituo vya polisi nchini viwe sawa muda wote.
“Hamjui siku wala saa ambapo
nitakuja, tufanye kazi, tuwahudumie wananchi, tusiwaonee wananchi,
tujitume kufanya kazi kwa weledi, sitamvumilia mtu ambaye atavunja
utaratibu,” alisema Lugola.
No comments :
Post a Comment