Afisa
Muandamizi wa Masoko Benki ya Watu wa Zanzibar Limited Ndg. Mohammed
Ismail Khamis,akimkabidhi msaada wa mchele kilo Elfu mbili (Tani 2) Mkuu
wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa kwa ajili ya
Kambi ya Wanafunzi wa Skuli za Wilaya ya Kusini Unguja wanaojiandaa kwa
Mitihani yao ya Taifa ya Kidatu cha Nne, inayotarajiwa kuaza wiki ijayo
Tanzania kote, makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa
Wilaya Kusini Unguja Makunduchi.
Mkuu
wa Wilaya Kusini Unguja Mhe Idrisa Kitwana Mustafa akitowa shukrani kwa
Uongozi wa PBZ,kwa msaada wao huo kwa ajili ya matumizi ya chakula
Wanafunzi wa Skuli za Wilaya ya Kusini wanaojiandaa na Mitihani yao ya
Taifa ya Kidatu cha Nne wiki ijayo, hafla hiyo imefanyika katika viwanja
vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.
Mkuu
wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya Wanafunzi wa Wilaya yake
katika kujiandaa na Mitihani yao ya Taifa ya Kidatu cha Nne, na kutowa
maelezo Wanafunzi hao wamejiandaa na kuweza kufanya vizuri mitihani hiyo
na kuibuka na division za kwanza kwa mwaka huu 2018.
Afisa
Muandamizi wa Masoko wa PBZ Ndg. Mohammed Ismail Khamis akizungumza na
Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe. Idrisa Ismail Khamis baada ya
kumalizika kwa hafla ya kukabidhi msaada wa mchele tani mbili, katika
viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Makunduchi Zanzibar.
Imeandaliwa na Blog ya Zanzinews.com.
Othman Mapara.
0777424152.
No comments :
Post a Comment