Uber yazindua Zana ya Usalama kwa abiria na madereva
|
JOHANNESBURG, South Africa, October 19, 2018/ -- Uber
(www.Uber.com) yaongezea usalama na yatoa Zana ya Usalama kwa abiria na
madereva katika nchi 8, pamoja na Tanzania; Vipengele vitajumuisha
Kituo cha Usalama, Waasiliani Wanaoaminika, kitufe cha usaidizi wa
dharura na taarifa kuhusu viwango vya mwendo ambavyo unaweza kuvigeuza
kukufaa.
Hivi leo Uber
imetangaza Zana mpya ya Usalama ambayo, kwa wiki chache zifuatazo,
itaanza kutumiwa na mamilioni ya abiria, madereva na watoa huduma ya
uwasilishaji wanaotumia programu hii katika bara Ulaya, Mashariki ya
Kati na Afrika. Zana hii itaanzisha vipengele vipya bunifu ambavyo
vinalenga kuimarisha kigezo cha usalama, na kuongezea uwazi, uwajibikaji
na kuwapa watumiaji wote utulivu wa akili.
Tangu
kuzinduliwa kwa programu hii, Uber imewapa mamilioni ya watu teknolojia
ambayo huwawezesha kupata gari kwa kubofya kitufe, kufuatilia kila
safari kwa kutumia teknolojia ya GPS na kuripoti matatizo yoyote 24/7
kwa timu yetu ya usalama. Kwa kuanzishwa kwa vipengele vipya vya
usalama, kampuni hii inalenga kuimarisha usalama na kusaidia kufanya
jamii ya Uber kuwa salama.
Vipengele ambavyo vitaanzishwa kama sehemu ya zana mpya ya usalama wa abiria na dereva, ni pamoja na:
Vipengele
hivi vipya vya usalama vitatolewa kwa awamu, sio abiria, madereva au
watoa huduma wote wa uwasilishaji wataweza kufikia vipengele hivi mara
moja.
“Na
zaidi ya safari milioni 15 kwenye programu ya Uber kila siku, hakuna
chochote muhimu kama usalama wa abiria, madereva na wasafirishaji.
Katika mwaka uliopita tumekuwa tukishughulikia kukuza bidhaa bunifu
ambazo zinaimarisha uwazi, uwajibikaji na utulivu wa akili kwa watumiaji
wote. Utoaji wa vipengele vyetu vipya vya Zana ya Usalama katika bara Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika ndio hatua inayofuata katika kuhakikisha kwamba tunamsaidia kila mtu kuwa salama na ameunganishwa, mahali popote alipo,” alisema Sachin Kansal, Mkuu wa Bidhaa za Usalama za Uber.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Uber Khosrowshahi amefanya usalama kuwa kipaumbele cha
juu cha 2018. Tangu kujiunga na kampuni, tumeanzisha mabadiliko kadhaa
duniani kote ikiwa ni pamoja na Kuwalinda madereva, abiria, na watoa
huduma wa uwasilishaji dhidi ya Majeraha, viwango vya saa vya dereva ili
kumsaidia kuzuia kuendesha gari akiwa ameduwaa, na Dereva Shiriki
Safari Yangu.
|
Pages
Saturday, October 20, 2018
Uber yazindua Zana ya Usalama kwa abiria na madereva
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment