Msanii Mesen Selekta na Gutta
wakionesha uwezo wao wa kutawala jukwaa kwenye Tamasha kubwa la Tigo
Fiesta -Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Nang’wanda Mjini Mtwara
usiku wa kuamkia Jumatatu
Mshindi atakayeiwakilisha Mtwara
kwenye kinyang’anyiro cha kumsaka Tigo Fiesta Supa Nyota, Siraji Mbuta
a.k.a Mbuta The Swagx akionesha uwezo wake kwenye jukwaa la Tigo Fiesta
usiku wa kuamkia jumatatu.
Msanii Bright akionesha uwezo wake
wa kutawala jukwaa kwenye Tamasha kubwa la Tigo Fiesta -Vibe Kama Lote
lililofanyika uwanja wa Nang’wanda Mjini Mtwara usiku wa kuamkia
Jumatatu
Msanii Chegge akionesha uwezo wake
wa kutawala jukwaa kwenye Tamasha kubwa la Tigo Fiesta -Vibe Kama Lote
lililofanyika uwanja wa Nang’wanda Mjini Mtwara usiku wa kuamkia
Jumatatu
Msanii Lulu Diva akionesha uwezo
wake wa kutawala jukwaa kwenye Tamasha kubwa la Tigo Fiesta -Vibe Kama
Lote lililofanyika uwanja wa Nang’wanda Mjini Mtwara usiku wa kuamkia
Jumatatu
……………………………
Msanii Jerry Boniface maarufu kama
Mesen Selekta akishirikiana na mdogo wake Gutta waliweza kuwapagawisha
mashabiki kwa mtindo wao Singeli.
Msanii huyo alidhihirisha ubora wake uliopelekea uwanja kutimka vumbi kwa nyimbo zake za Kinanda, Kanyaboya, Dab Singeli na nk.
Mji wa Mtwara ulikuwa tofauti na miji mingine kutokana na wasanii kuimba pamoja na mashabiki.
Akizungumza na waandishi wa habari
Mesen Selekta alisema ” Hii inanipa mzuka kwa mashabiki kuukubali
muziki wangu, nimeona jinsi shangwe la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote
walivyolipokea wana Mtwara”.
Msanii mwingine aliyeiteka Mtwara
alikuwa Farid Kubanda Fid Q aliwaamsha kwa wimbo wake Fresh, ambao
aliurudia mara mbili kutokana na kiu ya mashabiki.
Kivutio kingine kilikuwa kwa MaDj
Zero na Mafuvu waliweza kupiga mziki kwa zamu kama kwa kushindana hii
iliweza kuleta ladha na Vibe la aina yake kwa mashabiki.
Kila Tamasha linapopita utafutwa
msanii Chipukizi kupitia shindano la kusaka vipaji vya wasanii maarufu
Kama Tigo Fiesta Supa Nyota, na kwa mkoa huo msanii, Siraji Mbuta kwa
jina la kisanii Mbuta The Swagx aliibuka kidedea kuwakilisha mkoa huo
kwenye fainali mwezi ujao.
Kwa upande wa wadhamini Kampuni ya
Tigo, Meneja wa Kanda ya Pwani, John Tungaraza alisema ‘Mbali na
muziki, wateja wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi mara mbili ya thamani
kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia *147*00#. Promosheni
ya Data Kama Lote itahakikisha kuwa mashabiki wanaweza kufuatilia habari
na matukio yote ya msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote; au
kufurahia kuperuzi kwenye mtandao wenye kasi zaidi wa 4G+,’ Tungaraza
alisema.
Wateja wote wa Tigo pia wanaweza
kuvuna hadi TSH 10 millioni, zawadi za kila wiki za TSH milioni moja,
ama zawadi za kil asiku za TSH 100,000 kwa kushiriki katika shindano la
Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo. Ushiriki katika shindano hilo
unapatikana kwa kutuma neno MUZIKIkwenda 15571 au kwa kutembelea tovuti
ya http://tigofiesta.co.tz.
Walioshusha vibe kama lote mjini
Mtwara ni pamoja na kundi la Rostam (Roma and Stamina), Fid Q, Zaid na
Weusii (Joh Makini, Niki wa Pili na G-Nako) ambao walikonga mioyo ya
wapenzi wa muziki mjini Songea pia. Wengine ni wasanii wa bongo flava
Mesen Selekta na Foby, wakongwe Chegge, Barnaba na Mr Blue, pamoja na
akina dada Ruby na Lulu Diva.
TIketi za Tigo Fiesta 2018 –
zitakuwa zinapatikana kupitia Tigo Pesa Masterpass QR kwa kupiga
*150*01#, kuchagua namba 5 (lipia bidhaa), na kuchagua namba 2 (lipa kwa
Masterpass). Tuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.
Ijumaa ijayo Vibe litahamia Moshi Mjini
No comments :
Post a Comment