Mku wa maswala ya kibiashara wa
FINCA microfinance bank Emmanuel Mongella (kulia na mkuu wa idara ya
masoko na mawasiliano wa benki hiyo Nicholous John wakiongea na waadishi
wa habari katika uzinduzi wa programu ya Kuza ofisi na FINCA ilioanza
kuonyeshwa na TVE jijini Dares salaam.
…………………………..
- Lengo la shindano la TV ni kutoa elimu ya fedha na biashara kwa wamiliki wa biashara ndogo ndogo
- Benki ya FINCA Microfinance inaendelea kuwa benki ambayo inahamasisha ushirikishwaji wa kifedha katika kipindi cha miaka 20 na zaidi ya uwepo wake nchini Tanzania.
Tarehe 29 Septemba, 2018, Dar
es Salaam – Benki inayokua kwa kasi zaidi nchini Tanzania, Benki ya
FINCA Microfinance leo imezindua shindano la runinga ambalo lina lengo
la kuwaongezea uwezo wajasiriamali wadogo kwa kuwapatia stadi za
biashara, ufahamu na kisha kuwapatia zaidi ya TZS Millioni 10 kwa wazo
bora la biashara litakalokuwa limewasilishwa.
Awali Shindano hilo linalojulikana
kama ‘Kuza Ofisi na FINCA’ lilifanyika katika wilaya 4 za mkoa wa Dar
es salaam, Kinondoni, Ilala, Temeke na Ubungo. Wilaya hizi
zimeunganishwa kimkakati katika matawi ya benki yaliyoko Tegeta, Ilala,
Victoria na kando ya barabara ya Pugu kuelekea Uwanja wa Ndege.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa
program katika runinga jijini Dar es salaam, Mkuu wa Idara ya Masoko na
Mawasiliano wa Benki ya FINCA Microfinance bwana, Nicholous John alisema
kwamba lengo ni kuwapatia elimu ya biashara na fedha wamiliki wa
biashara ndogo ndogo ambao baadae itapelekea katika kukuza biashara zao.
Mshindi wa programu na shindano hili atawezeshwa kifedha kuendeleza
biashara zake ndogo ndogo.
“Hii ni Hatua ya pili la shindano
ambapo washindani 8 wamechaguliwa na jopo la majaji kushiriki katika
kipindi cha TV, ‘Kuza Ofisi na FINCA’ kitakachokuwa kinarushwa kupitia
TVE na kuendeshwa na mtangazaji wa Efm Emamnuel Kapanga. Mwishoni mwa
shindano, mshindi mmoja mwenye bahati ataondoka na zawadi nono ya zaidi
ya TZS milioni 10”, Alisema Nicholous, akiongeza kwamba washiriki
wengine wenye vigezo pia watakuwa na nafasi ya kujipatia mikopo kutoka
benki hiyo.
Kwa upande wake, mkuu wa maswala
ya masoko wa benki ya FINCA Microfinance Benki, Emmanel Mongella
amesema: “Kampeni ya Kuza Ofisi na FINCA ni sehemu ya FINCA
kusherehekea miaka 20 ya uendeshaji wa shughuli zake nchini Tanzania
ambapo benki ya FINCA imekuwa maarufu kwa utoaji wa masuluhisho bora na
aina mbalimbali za akaunti, Mikopo na huduma zingine ambazo zinajumuisha
mahitaji ya watu binafsi na taasisi.”
Emmanuel pia alisema,
“Ushirikishwaji wa Kifedha na Uvumbuzi wa Kidigitali ni msingi wa
biashara yetu, shindano hili ni ahadi nyingine ambayo Benki ya FINCA
Microfinance inatoa kwa watanzania kwamba iko kwaajili ya kuwasaidia
katika misaada ya kifedha kupitia elimu na kuwawezesha wateja wetu
kuweza kupata maendeleo endelevu ya biashara zao”.
Akizungumzia maono ya uzinduzi wa
programu hii John alisema, “nawasii watu wote waangalie programu hii
katika stesheni ya TVE maana kuna mambo mengi ya kufurahisha pamoja na
elimu ya biashara”
MWISHO//
Kuhusu FINCA
Kuhusu FINCA Microfinance Bank Tanzania
Benki ya FINCA Microfinance
Tanzania ni sehemu ya mtandao wa FINCA Impact Finance, Kundi la taasisi
zinazotoa mikopo midogo na taasisi za kifedha 21 ambazo zinatoa huduma
za kifedha kwa jamii na kusaidia wajasiriamali wenye kipato kidogo na
wamiliki wa biashara ndogo kuwekeza kwaajili ya baadae.
www.FINCA.co.tz
Kuhusu FINCA Impact Finance
Mtandao wa FINCA Impact Finance
wenye taasisi 21 za kutoa mikopo midogo na mabenki unatoa huduma za
kifedha za uwajibikaji ambazo zinawawezesha wajasiriamali wenye kipato
kidogo na wamiliki wa biashara ndogo kuwekeza kwaajili ya baadae.
Wamiliki wakuu wa mtandao huo ni FINCA International, watoaji wa mikopo
midogo midogo na kampuni yakijamii yasiyo ya kibiashara yaliyojikita
katika kujenga ushirikishwaji wa kiuchumi kwa watu maskini. Kwa maelezo
zaidi, Tembelea www.FINCAImpact.com.
……………………………………………………………………………………………………………
Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na:
Baraka Mosha,
Afisa Mahusiano na Mawasiliano kwa Umma
SIMU: 075696470
Barua pepe: Baraka.mosha@fincatz.org
www.FINCA.org
Twitter: @FINCA
No comments :
Post a Comment