Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tano ya
uelimishaji wa tathmini za ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo
na kazi kwa madaktari na watoa huduma ya afya wapatao 111 kutoka mikoa ya Kigoma, Tabora, Singida na Dodoma, yaliyokuwa yakiendeshwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi mjini
Singida, wakionyesha stika za utambuzi wa mtoa huduma (Daktari) kwenye vituo
vyao vya kazi, mwishoni mwa mafunzo hayo Septemba 28, 2018.

Mgeni rasmi, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Ernest
Mugeta, (katikati) akipeana mikono na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini
(WCF) Dkt. Abdulsalaam Omary, baada ya kufunga mafunzo hayo Septemba 28, 2018.
Kulia ni Mwenyekiti wa kundi la wataalam wa afya mahala pa kazi, Dkt. Robert
Mhina.

Meneja Madai na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi 9WCF), Dkt. Ali Mtulia akitoa mada.
Dkt. Pascal Mages, kutoka WCF akiwasilisha mada ya namna kwa wajumbe
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi,
Bi. Laura Kunenge, (Kulia), akimkabidhi stika ya utambuzi wa mtoa
huduma, mshiriki kutoka Mkoani Dodoima Dkt. Rehema Sovela, mwishoni mwa
mafunzo hayo.
Mkurugenzi
wa Huduma za Tiba na Tathmini, WCF, Dkt. Abdulsalaam Omary, akitoa hotuba ya
ukaribisho.

Baadhi ya washiriki wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi.
Mgeni
rasmi, Dkt.Ernest Mugeta, (kushoto), akimkabidhi cheti cha ushiriki,
Dkt.Mushi kutoka hospitali ya Rufaa ya Maweni Mkoani Kigoma.
Mgeni
rasmi, Dkt.Ernest Mugeta, (kushoto), akimkabidhi cheti cha ushiriki,
Dkt.Upendo Mabongo, kutoka kituo cha afya Kibakwe Mkoani Dodoma
Picha ya pamoja meza kuu na madaktari kutoka Mkoa wa Kigoma
Picha ya pamoja meza kuu na madaktari kutoka Mkoa wa Tabora.
Picha ya pamoja meza kuu na madaktari kutoka Mkoa wa Dodoma
Picha ya pamoja meza kuu na madaktari kutoka mkoa wa Singida.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Singida
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Singida
MFUKO
wa Fidia kwa Wafanyakazi WCF umefanikiwa kutoa mafunzo kwa madaktari na watoa
huduma ya afya wapatao 765 nchini nzima Tanzania Bara, Mkurugenzi wa Huduma za
Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omary, amesema.

Dkt.
Omary ameyasema hayo leo Septemba 28, 2018 mwishoni mwa mafunzo ya siku tano ya
uelimishaji wa tathmini za ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo
na kazi kwa madaktari na watoa huduma ya afya wapatao 111 kutoka mikoa ya
Kigoma, Tabora, Singida na Dodoma yaliyokuwa yakifanyika kwenye chuo cha
Uhasibu Mkoani Singida.

“Katika
kipindi hiki cha miaka miwili ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko kupokea madai
na kulipa mafao ya fidia, tayari tumetoa elimu kwa madaktari na watoa huduma ya
afya 765 na haya ni mafanikio makubwa katika suala zima la kufanya tathmini
iliyo sahihi ili hatimaye mfanyakazi mwenye madai aweze kulipwa fidia stahiki.”
Alibainisha Dkt. Omary. Alisema

elimu waliyoipata washiriki hao itawaweka kwenye nafasi nzuri ya kutoa haki kwa
pande zote mbili, mfanyakazi (mdai fidia) na Mfuko wenyewe kwani sasa wataweza
kufanya tathmini ya ulemavu (impairment assessment) inayozingatia muongozo na
misingi ya sharia.
Kwa
mujibu wa sheria, Mfuko ili uweze kulipa mafao ya fidia kwa mfanyakazi aliyepata
ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi, ni budi daktari
amfanyie tathmini ya kiwango cha maumivu au jeraha lililopelekea ulemavu uwe ni
wa muda au wa kudumu, lakini pia daktari atafanya tathmini kwa mfanyakazi
aliyepata maradhi yatokanayo na kazi ili hatimaye matokeo ya tathmini hiyo
ndiyo yatakayotumiwa na wataalamu wa Mfuko katika kufikia maamuzi ya kulipa
fidia kwa muhusika.

Aidha
Mfuko pia unajukumu la kulipa fidia kwa wategemezi wa Mfanyakazi aliyefariki
akiwa anatekeelza wajibu wake wa kazi.

Akiahirisha
mafunzo hayo, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Ernest Mugeta, alisema
ni matarajio ya mafunzo kwa washiriki kufanya kazi kwa uadilifu wa hali ya juu
na pasiwepo ushawishi wa mali au fedha ili haki itendeke.

“Nawaasa
ndugu zangu madaktari, haya mafunzo mliyoyapata, mkatumie ujuzi huo kwa makini.
Ninyi sasa ni wataalamu mliobobea ili kuusaidia Mfuko kufikia malengo
yaliyokusudiwa.” Alisema Dkt.

Mugeta. Aliwaomba
madaktari kufanya kazi hiyo ya tathmini kwa umakini wa hali ya juu kwani
matokeo ya tathmini hiyo yanahusu maisha ya mtu, kwa vile taarifa ya tathmini
ndiyo itakayotumiwa na Mfuko kutoa fidia kwa muhusika. Alitahadharisha
kuwa daktari au mtoa huduma ya afya, endapo atafanya kazi hiyo ya tathmini
kinyume cha sheria, basi ajue kuwa amevunja sheria na anaweza kushtakiwa. Akitoa
shukrani, kwa niaba ya washiriki wengine, Dkt.Yohana Masonda, alisema, mafunzo
hayo yatakuwa nyenzo bora katika utendaji wao wa kazi kwani sasa wamepata
uelewa wa namna ya kufanya tathmini ya ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa
yatokanayo na kazi.

Alisema
kabla ya mafunzo hayo walikuwa wakifanya akzi hizo sio kwa utaalamu sana ama
umahiri na kwamba faida za mafunzo kwao ni kutoa tathmini nzuri kwa waathirika
wa ajali au magonjwa yatokanayo na kazi.

No comments :
Post a Comment