Tuesday, September 18, 2018

WAZIRI KAMWELWE: SINA IMANI NA MHANDISI MSHAURI


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya LEA International Bw. Sanjeev Gupta (kushoto) anayesimamia ujenzi wa barabara ya Usesula-Komanga yenye urefu wa KM 108 kwa kiwango cha lami, wakati akikagua hatua za ujenzi wa barabara hiyo na kutoridhishwa na madaraja na makalvati yaliyotengenezwa katika mradi huo, mkoani Tabora.
Fundi Mchundo Bw. Fadhili Amiri, akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (wa pili kushoto) kuhusu kazi anazozifanya  wakati alipokuwa akikagua hatua za ujenzi wa barabara ya Usesula-Komanga yenye urefu wa KM 108 kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akikagua mchanga unaotumika kutengenezea madaraja na makalvati katika ujenzi wa barabara ya Usesula-Komanga yenye urefu wa KM 108 kwa kiwango cha lami, na kutoridhishwa na ubora wake, mkoani Tabora.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (wa kwanza) akisisitiza jambo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya SAMOTA Bw. Abdallah Salim, kuhusu kukamilisha mradi huo kwa wakati, mara baada ya kukagua hatua za maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28, Mkoani Tabora.


Muonekano wa sehemu ya  barabara ya Usesula-Komanga yenye urefu KM 108 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora. Mradi wa ujenzi huo utakamilika mwezi Machi mwaka 2021.

No comments :

Post a Comment