Kaimu meneja wa Shirika la umeme
Mkoa wa Pwani (TANESCO) Selemani Mgwila kushoto akimkabidhi msaada wa
mashuka 150 Mganga mkuu wa hospitali teule ya rufaa ya Mkoa wa Pwani
Tumbi Edward Wayi ambao umetolewa na Cha chama cha ushirika cha
wafanyakazi wa shirika la umeme Tanzania.
Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa
ya Mkoa wa Pwani Tumbi Edward Wayi kushoto akisalimia na Kaimu meneja wa
Shirika la umeme Tanesco Mkoa wa Pwani Selemani Mgwila mara baada ya
halfa ya kukabidhiwa mashuka 150 kwa ajili ya wagonjwa.
Mjumbe wa bodi wa chama cha
ushirika cha wafanyakazi wa shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Mussa
Chowo akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa halfa
hiyo ya makabidhiano ya mashuka.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) wakiwa katika halfa hiyo ya makabidhiano ya mashuka.
VICTOR MASANGU, PWANI
HOSPITALI teule
ya rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi kwa sasa inakabiliwa na changamoto mbali
mbali ikiwemo upungufu wa mashuka,vifaa tiba, pamoja na uchakavu
mkubwa wa
miundombinu wa majengo hivyo kupelekea kupelekea usumbufu
mkubwa kwa wagonjwa pindi wanapoitaji huduma kwa ajili ya kupatiwa
matibabu.
Hayo
yamebainishwa na Mganga mkuu wa hospitali hiyo Edward Wayi wakati wa
halfa fupi ya kukabidhiwa msaada wa mashuka 150 kutoka kwa chama cha
ushirika cha wafanyakazi wa shirika la umeme Tanzania (TANESCO) na
kuhudhuliwa na wadau mbali mbali wa maendeleo katika sekta ya afya.
Wayi amesema
kwamba kwa sasa katika hospitali hiyo ambayo ina jumla ya vitanda 254
hivyo bado kuna uhitaji mkubwa wa mashuka kwa ajili ya wagonjwa na
kuongeza kuwa msaada huo walioupata kutoka Tanesco utaweza kusaidia kwa
kiasi kikubwa katika kuboresha huduma kwa wagonjwa ambao wanakwenda
kupatiwa matibabu.
Kwa upande wake
Kaimu meneja wa Tanesco Mkoa wa Pwani Seleman Mgwila alisema kwamba
lengo kubwa la kusaidia katika hospitali ya tumbi ni kutokana na utafiti
ambao waliufanya na kubaini kuwepo kwa changamoto kubwa ya upungufu wa
mashuka hivyo wameamua kutoa msaada huo wa mashuka 150 ambayo yatasaidia
kupunguza kero ambayo waliyokuwa wakiipta wagonjwa hususan majeruhi wa
ajali za barabarani.
“sisi kama
Tanesco Saccos tulifanya utafiti tukaona kuna changamoto kubwa katika
sekta ya afya hususan kwa wagonjwa kupata shida ya mashuka, hivyo sisi
tukaona kuna umuhimu mkubwa wa kutoa msaada wa mashuka katika hospitali
hii ya Rufaa ya Mkoa tumbi, kwa sasa tayari tumeshatoa mashuka kwa
hospitali zote za Mkoa kwa nchi nzima,”alisema Mgwila.
Naye mjumbe wa
bodi kutoka Tanasco Saccos Mussa Chowo alibainisha kuwa lengo lao kubwa
ni kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano Dk, John Pombe Magufuli
katika kuboresha sekta ya afya ambapo amebainisha kuwa kwa sasa
wameshatoa msaada wa mashuka katika hospitali zote za Mkoa Tanzania
nzima ili kuisaidia jamii katika suala zima la kupata huduma bora .
No comments :
Post a Comment