Waziri wa Biashara na
Viwanda, Charles Mwijage (katikati) akishikana mikono na Meneja wa NBC
Kanda ya Ziwa, Japhet Mazumira, wakati akitembelea banda la
benki hiyo katika maonyesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya
Madini yanayoendekea katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita leo.
kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Gabriel Robert na wa pili kulia ni
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin
Rutageruka. NBC ni mdhamini mkuu wa maonyesho hayo.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akipokewa na
Meneja wa NBC Kanda ya Ziwa, NBC, Japhet Mazumira (kulia), wakati
akitembelea banda la benki hiyo katika maonyesho ya Teknolojia na
Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoedelea katika Viwanja vya CCM
Kalangalala mjini Geita leo. Kutoka ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Gabriel
Robert.
Ofisa Mahusiano ya
Wateja wa Benki ya NBC Tanzania, Esther Kahabi akizungumza na wachimbaji wadogo
wa madini katika Kliniki ya Biashara ya NBC iliyooandaliwa na benki
hiyo kwa kushirikiana na TanTrade katika maonyesho hayo. NBC ni mdhamini
mkuu wa maonyesho hayo
Waziri wa Biashara na
Viwanda, Charles Mwijage (kushoto) akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa
Benki ya NBC, wakati akitembelea banda la benki hiyo katika maonyesho
ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayofanyika katika
viwanja vya CCM Kalangalala Mkoani Geita leo. NBC ni mdhamini mkuu wa maonyesho
hayo.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe (katikati) akisaini kitabu cha wageni
katiba banda la Benki ya NBC wakati akitembelea banda hilo wakati wa maonyesho
ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayondelea katika
Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita,
Mhandisi Gabriel Robert na kushoto ni Meneja wa NBC Kanda ya Ziwa, Japhet
Mazumira. NBC ni mdhamini mkuu wa maonyesho hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka
(kushoto) akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini kutoka Mkoa wa Geita
wakati wa Kliniki ya Biasharaya NBC iliyooandaliwa na benki hiyo kwa
kushirikiana na TanTrade wakati wa maonyesho ya Teknolojia na Uwekezaji
kwenye Sekta ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini
Geita. Kushoto kwake ni, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Gabriel Robert na
Mwenyekiti wa Chama Cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Geita (GEREMA), Michael Kadeo.
NBC ni mdhamini mkuu wa maonyesho hayo
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Gabriel Robert akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini wakati wa Kliniki ya Biashara ya NBC iliyooandaliwa na benki hiyo kwa kushirikiana na TanTrade ili kuwapa mbinu wa ujuzi katika biashara zao wakati wa maonyesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala Mkoani Geita. NBC ni mdhamini mkuu wa maonyesho hayo.
No comments :
Post a Comment