Serikali
inakamilisha zoezi la uhakiki wa maeneo yaliyotengwa na mikoa kwa ajili
ya shughuli za vijana ili kutekeleza mpango wa kuwawezesha vijana
vitalu nyumba na mafunzo ya kutengeneza vitalu nyumba.Mpango huu
utaifikia mikoa 7 katika hatua ya mwanzo na baadaye kuifikia mikoa mingi
zaidi hasa kutokana na utayari wa mikoa husika katika kutenga maeneo ya
kilimo kwa Vijana.
Hayo
yamesemwa Septemba 18, 2018 mkoani Simiyu na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (pichani
anayemwagilia) wakati akikagua maeneo yaliyotengwa kwa kilimo cha Vijana
katika kijiji cha Mwamanyili-Wilaya ya Busega,Nyakabindi-Wilaya ya
Bariadi na Kijiji cha Ngh’eshi-Wilaya ya Itilima,ambapo ameeleza dhamira
ya Serikali ya kuwawezesha vijana katika kilimo ili kupunguza
changamoto za Ajira kwa Vijana.
Naibu
Waziri Mavunde pia amelipongeza Shirika la World Vision kwa
kushirikiana na Mbunge wa Itilima Mh Daud Silanga Njalu kwa ujenzi wa
kituo cha Maarifa ambacho kinawapatia Vijana mafunzo ya fani mbalimbali
za Ufundi.
Wakati
huo huo Mh Mavunde,amewataka uongozi wa Wilaya ya Halmashauri ya
Itilima kuwapa zabuni ya kufyatua matofali ya ujenzi wa zahanati kwa
vikundi vya Vijana kama njia ya kuviwezesha kufikia mafanikio yao ya
kiuchumi.






No comments :
Post a Comment