Sunday, September 30, 2018

SERIKALI KULETA MABADILIKO YA KIUCHUMI KWA WAFANYAKAZI

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na Viongozi wanawake kutoka vyama vya wafanyakazi Mkoani Morogoro kuhusu kuwahimiza wafanyakazi kuchangamkia fursa za shughuli za kimaendeleo zilizopo nchini.

  Rais wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamuhoke akielezea jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipokutana kwa lengo la kuzungumza na Viongozi Wanawake kutoka kwenye Vyama vya Wafanyakazi Mkoani Morogoro.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’i Issa akizungumzia Sera ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa viongozi kutoka vyama vya wafanyakazi walipokutana Mkoani Morogoro.
Baadhi ya viongozi kutoka kwenye Vyama mbalimbali vya Wafanyakazi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipokutana nao kuzungumzia ushirikishwaji wa wafanyakazi kwenye dhana ya uchumi wa viwanda.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza jambo na Rais wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamuhoke kuhusu kuwawezesha wafanyakazi kushiriki katika mipango ya maendeleo ya taifa. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake (TAMIKO) Bi. Veneranda Seif.
Baadhi ya viongozi kutoka kwenye Vyama mbalimbali vya Wafanyakazi wakifuatilia kwa makini mkutano huo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb)
Meneja Kanda ya Kati kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Bw. George Nyamrunda akielezea kuhusu mikopo ya kilimo inayotolewa na benki ya maendeleo ya kilimo.(PICHA:OWM-KVAU)

No comments :

Post a Comment