Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi
Balozi John Kijazi akifungua Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu
Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia
Septemba 19,2018.
Mtendaji Mkuuwa Taasisi ya Uongozi
Prof. Joseph Semboja akisistiza jambo wakati wa Kikao kazi cha
Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma
kwa siku tatu kuanzia Septemba 19,2018.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya
Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Bw. James Syanga akiwasilisha mada
kuhusu athari za madawa ya kulevya wakati wa Kikao kazi cha Makatibu
Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku
tatu kuanzia Septemba 19,2018.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Bi Susan Mlawi akijitambulisha wakati wa wa
Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika
Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19,2018.
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Bw.
David Kafulila akijitambulisha wakati wa wa Kikao kazi cha Makatibu
Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku
tatu kuanzia Septemba 19,2018.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Nichalaus William akijitambulisha
katika kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa
kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19,2018.
Sehemu ya Makatibu Wakuu
wakifuatilia uwasilisjhaji wa mada mbalimbali kwenye Kikao kazi cha
Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma
kwa siku tatu kuanzia Septemba 19,2018.
Manaibu Katibu Wakuu na Makatibu
Tawala wakifuatilia mada wakati wa Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na
Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu
kuanzia Septemba 19,2018.
Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi
Balozi John Kijazi akiwa kwenye picha ya pamoja na Makatibu Wakuu mara
baada ya kufungua kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa
Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba
19,2018.
Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi
Balozi John Kijazi akiwa kwenye picha ya pamoja na Makatibu Tawala wa
Mikoa mara baada ya kufungua Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu
Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia
Septemba 19,2018.
Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi
Balozi John Kijazi akiwa kwenye picha ya pamoja na watoa mada wa Kikao
Kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika
Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19,2018 wakiwemo Makatibu
Wakuu.
Sehemu ya washiriki wa Kikao Kazi
cha Makatibu Wakuu wa Wizara na Makatibu Tawala wa Mikoa wakifuatilia
kikao kazi chao kinachoendelea Jijijini Dodoma. (Picha zote na Frank
Shija- MAELEZO)
Na: Frank Mvungi- MAELEZO
Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi
Balozi John Kijazi amewataka Makatibu Wakuu wa Wizara na Makatibu Tawala
wa Mikoa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria , Kanuni,
Taratibu na Miongozo inayotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano kila
wanapofanya maamuzi.
Akizungumza leo Jijini Dodoma
wakati akifungua kikao kazi cha siku tatu kwa Viongozi hao Balozi Kijazi
amesema kuwa wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa wanazingatia
taratibu zote ili azma ya kujenga uchumi wa viwanda ifikiwe kwa wakati
na kuwanufaisha wananchi.
“Nafasi zenu ni za maamuzi hivyo
msipofanya maamuzi sahihi na kwa wakati mtakwamisha shughuli za
maendeleo na huduma muhimu kwa wananchi.” Alisisitiza Mhandisi Kijazi.
Akifafanua, Mhandisi Kijazi
amesema kuwa wajumbe wa mkutano huo wanalojukumu kubwa la kuhakikisha
kuwa wanafanyia kazi masuala yote yatakayoazimiwa katika kikao kazi
hicho cha siku tatu kinacholenga kuongeza tija katika ngazi ya Wizara na
Mikoa kwa kuzingatia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano yakuleta mageuzi
makubwa katika nyanza zote hasa katika huduma zinazotolewa kwa
wananchi.
Aliongeza kuwa Kikao kazi hicho
kina umuhimu mkubwa na kitakuwa kikifanyika kila mwaka ili kuwapa fursa
Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala kubadilishana uzoefu, kubaini
changamoto zilizopo na kuweka utaratibu mzuri wa kuzitatua kwa maslahi
ya wanachi.
Akizungumzia mabadiliko
yaliyofanywa na Serikali Balozi Kijazi amesema kuwa ni pamoja na kuwepo
kwa muundo mpya kwa Wizara zote unaoendana na mahitaji na mipango ya
Serikali ya Awamu ya Tano utakowezesha kutatutuliwa kwa changamoto
zilizokuwepo kabla ikiwemo kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.
Kauli mbiu ya Kikao kazi hicho ni
“Uongozi makini na wapamoja unaozingatia uzalendo, uwajibikaji,
utawalabora na kusimamia rasilimali zetu ni nyenzo muhimu katika
kuifikisha Tanzania katika uchumi wa Kati” Alisisitiza Balozi Mhandisi
Kijazi.
Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu wa
Wizara, Makatibu Tawala wa Mikoa Kinafanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu
kikilenga kuimarisha na kuongeza tija katika kuwahudumia wananchi kama
ilivyo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John
Pombe Magufuli.
No comments :
Post a Comment