Na Christian Gaya, majira 28 Septemba 2018
Pamoja
na juhudi zote za kuboresha uelewo wa umuhimu wa hitaji la kuwa na bima
miongoni mwa watanzania kiwango cha wigo wa soko la bima bado kipo chini sana ingawa wadau wengi wana wanategemea ya kuwa uwingo wa watu kuwa na bima utaongezeka.
Kwa umuhimu wa sekta ya bima kwa aina yeyote ya
uchumi, hasa kama ulinzi kwa biashara na watu wenyewe kwa majanga hatarishi
imekuwa ni kero sana kwa wadau na kusababisha kuwa ndiyo chanzo cha matatizo.
Ingawa baadhi ya wadau wa sekta ya bima wanasema kuna maendeleo kidogo katika sekta
hii.
Kwa
takwimu zilizopo inaonesha uwigo wa bima hapa nchini upo chini ya asilimia moja
na mchango wake kwa pato la taifa bado uko chini pia kwa mwaka. Kwa mfano kwa
mwaka unaoshia 31Desemba 2016, sekta ya bima nchini iliongezeka kwa asilimia
7.0 kutoka shilingi bilioni 618.9 fedha za Kitanzania mpaka kufikia shilingi
bilioni 660.0 za Kitanzania
Uwigo
huu wa soko la bima kuwa kidogo, unalalamikiwa kuchangiwa na sababu mbalimbali.
Na mojawapo ya sababu kubwa zimekuwa ni kuwa na uelewo mdogo juu ya dhana nzima
la bima miongoni mwa watanzania, kipato kidogo cha watanzania cha kuweza
kununulia bima, utaratibu mbaya wa uendeshaji wa soko la bima, na kuwa na
bidhaa za bima zisizowavutia wateja.
Na
moja kubwa kabisa, kukosa nguvu ya serikali kutowekea mazingira mazuri na kipaumbele
kwa biashara ya bima hivyo kufanya kama kizuizi kikuu cha ukuaji wa bima
nchini.
Wauza
bima kukosa uaminifu miongoni mwa idadi kubwa ya Watanzania imekuwa ni sababu
mojawapo ya ukuaji mdogo wa uwigo wa biashara ya bima nchini. Taarifa
zinazopatikana zinaonesha ya kuwa Watanzania wengi wanaacha kukata bima kwa
sababu ya ugumu na usumbufu wa utaratibu wa madai wakati maafa hatarishi
yakitokea au wakati bima yake imeshaiva tayari.
Ingawa
jambo hili kwa kiasi kikubwa limeweza kuingiliwa kati na kutatuliwa kwa
mshirikiano mkubwa na watoa bima na msimamizi wa bima yaani kamishna wa bima
Tanzania (TIRA).
TIRA
kwa upande wake kama msimamizi wa bima nchini imeweza kutumia nguvu za kisheria
ilizopewa kuhakikisha ya kuwa kampuni za bima nchini zinafuata utaratibu na
kanuni pamoja na sheria zilizowekwa kwa ajili ya kumlinda mlaji na kwa manufaa
ya uchumi wa nchi kwa ujumla.
Kipingamizi
kikubwa cha bima hapa Tanzania hasa ni gharama ya juu ya bei ya vifurushi vya
bima. Na kwa wale wanaoilalamikia Serikali kwa bima kuwa na uwingo kidogo
nchini, wanasema serikali ambayo ina msingi wa rasilimali nyingi na kubwa mara
nyingi inakatia bima ila inakuja kutifua kwa upande wa bei za bima na ulipaji
wake.
Utafiti
unaonesha ya kuwa sekta ya bima haijaguswa kabisa, kwa sababu mpaka sasa
haijatumia vizuri sekta isiyo rasmi ambayo inashikiria karibu asilimia 90 ya
idadi yote ya watu wote wa hapa nchini.
Ambayo
hii ni mojawapo ya sababu kubwa ya ulazima wa kuanzisha bima kwa ajili ya kundi
hili kubwa la Watanzania ambao wako kwenye sekta isiyo rasmi ambao karibu wote
wanafanyia kazi zao kwenye mazingira hatarishi yasiyokuwa na bima ya aina
yeyote.
Kabla,
wadau katika sekta hii wamekuwa wakifanya bidii kubwa ya kutaka kubadilisha
mazungumzo hasi juu ya huduma za bima nchini. Na hii imekuwa ni matokeo ya kuwa
na sekta nzuri ya usimamizi wa bima, angalau uelewo zaidi juu ya bima za magari
unaongezeka kidogo.
Ili
kuleta mabadiliko yanayoeleweka katika sekta hii ya bima, wataalamu wengi
wanapendekeza baadhi ya hatua muhimu kuchukuliwa ambazo wanasema huenda
zinaweza kuboresha sekta. Wanazipigia debe sana kuanzishwa kwa bima
zinazolingana na mahitaji ya mteja mwenyewe kwa wakati huo, na bima ndogo kwa
ajili ya watu waliopo kwenye sekta isiyo rasmi na bima ya miiko au takaful.
Ikumbukwe
ya kuwa mwendelezo wa soko la bima ndogo ndogo ni mojawapo ya malengo ya
mwendelezo wa ukuzaji wa soko la bima yanayofanywa nchini, kwa malengo na mikakati
ya TIRA ambapo Kamishna wa Bima alianzisha na kuungwa mkono na wadau wa sekta kama
ndiyo mwanzo wa jambo wa kuanzia kuitangaza maendeleo ya sekta ya bima nchini. Inandelea wiki ijayo
No comments :
Post a Comment