Mtaalamu kutoka Kitengo cha
radiolojia (MAMC) akiwa anatoa elimu ya saratani ya matiti kwa wanawake
waliojitokeza kwenye zoezi hilo kabla ya kufanyiwa uchunguzi huo
Baadhi ya wanawake waliojiokeza
kwenye zoezi la uchunguzi wa saratani ya matiti wakiwa wanasubiri
kufanyiwa vipimo hospitalini hapo
Daktari akiwa anasikiliza maelezo kutoka kwa mgonjwa kabla ya kuanza kufanyiwa uchunguzi
Katika kuelekea mwaka mmoja wa
kutoa huduma Hospitali ya Rufaa Mloganzila (MAMC) imetoa huduma bure ya
uchunguzi wa awali ya saratani ya matiti kwa wanawake waliojitokeza
Hospitalini hapo.
Katika Huduma hii ya uchunguzi wa
awali wa saratani ya matiti wanawake waliweza kupata
elimu kuhusu
saratani nini, dalili za saratani ya matiti, vichochezi vya saratani ya
matiti, umuhimu wa kujichunguza na pia kuonyesha elimu ya vitendo ya
jinsi ya kujichunguza.
Akizungumza wakati wa zoezi hili,
Daktari Lulu Fundi Sakafu, Mtaalamu wa Radilojia kutoka Hospitali ya
Rufaa Mloganzila amesema. Huduma hii ni moja wapo ya shughuli tuliofanya
katika kuazimisha mwaka mmoja wa kutoa huduma na tumefanya huduma hii
bure kwa sababu ni muhimu kugundua saratani mapema na wagonjwa wengi
wanakuja hospitali wakiwa tayari tatizo limekuwa kubwa ndiyo maana
tumeamua kufanya zoezi hili kwa jamii yetu hasa wanawake.
Katika zoezi hili Zaidi
yawanawake130waliwezakupatiwahuduma hii na kati yao 37 waliweza
kugundulika kuwa na viashiria vya awali vya saratani ya matii.
No comments :
Post a Comment