Mwenyekiti
wa Kongomano la Wazee ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wazee
Tanzania Mzee Sebastian Bulegi akiongoza Wazee walioshiriki katika
kongomano la wazee kwa lengo la kujadili changamoto wanazokabiliana nazo
wazee nchini wakati wa kongamano la wazee kuelekea Siku ya Kimataifa ya
Wazee yatakayofanyika Jijini Arusha Oktoba Mosi.
Mratibu
wa huduma za Afya kwa Wazee kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Edward Mung’ong’o akiwasilisha mada wakati
wa kongomano kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee leo
Jijini Arusha.
Kamishana
wa Polisi akieleze kuhusu hali ya mauaji ya wazee nchini na hatua
zinazochukuliwa na jeshi hilo katika kupambana na vitebdo vya ukatili
kwa wazee wakati wa kongomano kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa
ya Wazee leo Jijini Arusha.
Wazee
walioshiriki Kongamano la Wazee wakifuatilia mada mbalimbali
zinazotolewa katika Kongamano hilo ikiwa ni moja ya shighuli
zinazofanyika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee
yatakayofanyika Jiji la Arusha Oktoba Mosi
Wazee
walioshiriki Kongamano la Wazee wakifuatilia mada mbalimbali
zinazotolewa katika Kongamano hilo ikiwa ni moja ya shighuli
zinazofanyika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee
yatakayofanyika Jiji la Arusha Oktoba Mosi
Kamishna
wa Ustawi wa Jamii Nchini Dkt. Naftali Ng’ondi akielezea lengo la
kongamano kwa wazee waliohudhuria kongamano la wazee kuelekea Siku ya
Kimataifa ya Wazee yatakayofanyika Jijini Arusha Oktoba Mosi.(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW)
Na Mwandishi Wetu -Arusha
Tanzania
inakadiliwa itakuwa na wazee 11% ya watu wote nchini ifikapo mwaka
2050, kwa kuwa idadi ya watu inaongezeka kwa kasi kutokana na kuendelea
kuboreka kwa huduma za Afya hapa nchini. Hayo
yamesemwa na Mratibu wa Huduma za Afya kwa Wazee kutoka Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Edward Mung’ong’o
wakati akiwasilisha mada kwenye kongomano lililofanyika leo Jijini
Arusha kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee, amesema kuwa
Mwaka 2002 idadi ya Wazee ilikuwa milioni 1.4, ikiwa ni sawa na 4% ya
watu wote yaani Milioni 33.5.
Aidha
Dkt. Mung’ong’o amesema kuwa kwa sasa idadi ya Wazee hapa nchini
inakisiwa kuwa milioni 3 sawa na 5.6% ya watu wote ambao kwa takwimu za
sasa Tanzania ina Watu milioni 55.
Akizungumzia
mafanikio ya serikali katika kuboresha huduma za Afya kwa Wazee Dkt.
Mung’ong’o amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na Shirika la HelpAge
International imepitia na kuboresha Mtaala wa kufundishia Wauguzi ngazi
ya kata ili wapate mafunzo yatakayowawezesha kuhudumia Wazee kwa
ufanisi.
Aidha
Dkt. Mung’ong,o aliongeza kuwa kwa kushirikiana na HelpAge
International pia serikali imeandaa Mwongozo kwa ajili ya watoa huduma
wa kuwaelekeza jinsi ya kutibu magonjwa ya kawaida yanayowasibu Wazee. Wakati
huo huo Kamishna wa Ustawi wa Jamii nchini Dkt. Naftali Ng’ondi
akifungua Kongamano hilo kwa niaba ya Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto alisema Wazee watatumia
fursa hiyo kujadiliana juu ya utekelezaji wa Sera na Miongozo ya
kuboresha hali na Maisha ya Wazee nchini kwa kuzingatia utambuzi wa
wazee katika Halmashauri, upatikanaji wa huduma za Afya kwa wazee na
ushirikishwaji wa wazee.
Aidha
Kamishna Ng’ondi aliwaeleza wajumbe wa Kongamano hilo kuwa mengine
yatakayojadiliwa ni Huduma za Afya kwa wazee na utekelezaji wa Mpango wa
huduma Rafiki wa Afya kwa Wazee na mabadiliko ya Utaratibu wa
Uchangiaji wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na azma ya Serikali Kufikia
Pensheni ya Jamii kwa Wazee wote.
Aidha
Dkt. Ng’ondi alisema kimsingi kongamano la Wazee pia litaangalia Sera
na Mfumo wa Kodi unavyozingatia mahitaji ya makundi Maalumu Msamaha kwa
Wazee hali ya Mauaji ya Wazee nchini na Jitihada za Kukabiliana na Hali
hiyo.
Kamishna
Ng’ondi alisema kuwa pamoja na umri mkubwa walionao wazee wana haki ya
kuheshimiwa utu wao na kupata haki zote wanazostahiki kama binadamu
ikiwa ni pamoja na haki ya kuishi, kupata matunzo katika familia na
kulindwa dhidi ya madhara yoyote yanayoweza kuwaathiri kimwili, kiakili,
kihisia na kisaikolojia. Wazee
wamekutana leo Jijini Arusha kushiriki kongamano la Wazee katika
kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee yanayofanyika kitaifa
Jijini Arusha kwa lengo kutoa fursa kwa wazee kujumuika kwa pamoja na
kujadili changamoto na fursa zilizopo katika kuboresha hali ya maisha
yao nchini Siku
ya Kimataifa ya Wazee huadhimishwa kufuatia Azimio la Umoja wa Mataifa
Namba 45/106 la mwaka 1990 linalozitaka nchi wanachama kutenga siku
maalumu ya kutafakari mchango wa Wazee katika maendeleo ya jamii.
No comments :
Post a Comment