Wednesday, August 1, 2018

KIGAMBONI WAPONGEZWA KWA KUJENGA OFISI YA KISASA


JAFO 1
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani
Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya Kigamboni katika eneo la ujenzi wa majengo
ya Ofisi ya Mkuu wa wilaya na Halmashauri ya Kigamboni.
JAFO 2
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani
Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya Kigamboni katika eneo la ujenzi wa majengo
ya Ofisi ya Mkuu wa wilaya na Halmashauri ya Kigamboni.
JAFO 3
Kazi ya ujenzi inavyoendelea
Kigamboni.
kigamboni (3)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akiendelea na zoezi la ukaguzi wa jengo la
Manispaa ya Kigamboni.
kigamboni (4)
Ukaguzi wa maendeleo ya jengo la Ofisi ya mkuu wa wilaya ya
Kigamboni.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo amewapongeza wilaya na Manispaa ya Kigamboni kwa kuanza ujenzi wa Ofisi za Kisasa.
Waziri Jafo ametoa pongezi hizo alipotembelea kukagua ujenzi wa Ofisi  ya Mkuu wa Wilaya pamoja na ujenzi wa Ofisi mpya za Manispaa ya Kigamboni.
Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amefurahishwa na ujenzi unaoendelea wilayani humo unaojengwa na Wakala wa Majengo(TBA) chini ya mkandarasi Mshauri kutoa Chuo cha Ardhi.
Jafo amewataka wakandarasi kukamilisha kazi hiyo ndani ya muda ili watumishi wa Manispaa ya Kigamboni wapate maeneo mazuri ya kufanyia kazi.
Naye, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Rahel Mhando amemuhakikishia Waziri Jafo kwamba viongozi wote wa Kigamboni wamejipanga vyema ili ujenzi huo ukamilike ndani ya muda uliopangwa.

No comments :

Post a Comment