Rais
Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemuwakilisha Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye
sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Zimbabwe Mhe. Emmerson Dambudzo
Mnangagwa zilizofanyika leo Jumapili Agosti 26, 2018 katika uwanja wa
michezo mjini Harare. Katika safari hiyo Dkt. Kikwete aliambatana na
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Bw.. Philip
Mangula akiwa na Mwenyekiti wa United Democratic Party (UDP) Bw. John
Momose Cheyo kama wanavyoonekana pichani wakiwa na mazungumzo na Rais
Mnangangwa jijini Harare baada ya sherehe za kuapishwa.
Rais Mnangagwa akiwa na mazungumzo na Dkt. Kikwete.
Dkt. Kikwete, akisalimiana na Katibu Mtendaji Mkuu wa SADC,Dr. Stergomena L. Tax kwenye uwanja wa michezo mjini Harare, Zimbabwe wakati wa sherehe za kuapishwa kwa Rais Mnangangwa.
JK akiwasili kwenye uwanja wa michezo wa
Harare tayari kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye sherehe za
kuapishwa kwa Rais Emmerson Mnangagwa.




No comments :
Post a Comment