Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiangalia pikipiki
zilizotolewa na wadau wa kupinga vita uhalifu kwa Kituo cha Polisi Muriet, kilichopo Kata ya
Muriet. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani
Ng’anzi.Waziri Lugola yupo jijini Arusha kwa ziara ya kikazi.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, Mrisho Gambo (kulia)
na Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani
Ng’anzi (kushoto) kutembelea Kituo cha
Polisi cha Muriet (kinachoonekana pichani) na nyumba za askari polisi zilizopo
katika eneo hilo wakati wa ziara yake jijini Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, akifafanua
jambo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola(wapili kushoto),
alipotembelea nyumba za askari polisi zinazoonekana pichani, katika eneo la
Kata ya Muriet,jijini Arusha.Kushoto ni
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Ramadhani Ng’anzi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola,
akizungumza na wananchi wa Kata ya Muriet, baada ya kutembelea Kituo cha Polisi na nyumba
za askari polisi zilizopo eneo hilo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
No comments :
Post a Comment