Nelson Goima
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame
Mbarawa amempa miezi minne mkandarasi anayejenga mradi wa visima virefu
vya Kimbiji na Mpera mkoani Dar es Salaam, kukamilisha kazi hiyo ili
wananchi wapate majisafi.
Pia, amempa wiki moja mkandarasi huyo, kampuni za NSPT ya Iran na Serengeti ya Tanzania, kuweka benki malipo ya awali ya dola milioni 1.5 na kuwawekea bima wafanyakazi, kama mkataba unavyotaka.
“Mkandarasi sitaki simu yako, ninachotaka ni maji tu na Watanzania wanachohitaji ni maji tu” amesisitiza Mbarawa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Serengeti, Ali Talbei na Mhandisi Mshauri, Dk Charles Kaaya wakati wakiwa eneo la Kimbiji.
Alikuwa akitembelea mradi wa kuchimba visima virefu Kimbiji, ikiwa ni sehemu ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa).
Mbarawa amesema mradi wa visima virefu Kimbiji na Mpera, ulianza mwaka 2013 na ulitakiwa ukamilike baada ya miezi 15, lakini haujakamilika hadi sasa kutokana na changamoto kadhaa.
Hivyo, Mbarawa alisema kwa sasa Serikali imeanzisha mpango wa kuokoa mradi huo, ambapo itasaidiana na mkandarasi, kujenga mradi huo usiku na mchana na kununua vifaa vya mradi kutoka viwanda vya Tanzania, badala ya kuagiza nje. “Visima 20 vikikamilika vitazalisha lita milioni 260 kwa siku.
Haya ni maji mengi sana, vikikamilika kutakuwa hakuna tatizo la maji. Maji ya visima hivi 20 ni nusu ya maji yanayozalishwa kwa pamoja na mitambo ya Ruvu Juu na Ruvu Chini, ambayo ni lita milioni 502 kwa siku”, alisema akiwa waziri huyo na viongozi wa Dawasa.
Visima vya Kimbiji na Mpera ni moja ya miradi ya kimkakati, inayotekelezwa na wizara hiyo kupitia Dawasa, yenye lengo la kuongeza wingi wa maji Dar es Salaam na maeneo jirani kutoka lita milioni 300 mpaka lita milioni 720, zitakazotosheleza mahitaji hadi mwaka 2032.
Kukamilika kwa visima hivyo 20, kutaimarisha upatikanaji wa maji katika maeneo ambayo hayana huduma nzuri ya majisafi na yale yasiyokuwa na mtandao rasmi.
Maeneo hayo ni Kigamboni, Kibada, Kisarawe Two, Kongowe, Gongolamboto, Segerea, Pugu, Chanika, Chamazi, Charambe, Buyuni, Mbagala, Makangarawe, Tazara, Ukonga, eneo la viwanda Barabara ya Nyerere, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Mwalimu Nyerere, Kiwalani, mji wa Mkuranga mkoani Pwani na vitongoji vyake mfano Kisemvule. Mradi huo wa Kimbiji na Mpera unatekelezwa kwa gharama ya dola za Marekani milioni 19.8.

No comments :
Post a Comment