Sunday, July 1, 2018

Video: Zitto, Polepole watunishiana misuli mtandaoni, ‘Mzee wa kurukia treni kwa mbele ushaanza’



Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe wameibua mvutano mkali katika mtandao wa kijamii wa ‘Twitter’. Katika mabadiliko hayo yaliyofanywa na Rais John Magufuli, Mwigulu Nchemba ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ameachwa. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Zitto aliandika kuwa;
“Ndugu yangu Mwigulu Nchemba karibu back bencha ufanye kazi ya wananchi. Tunajua msimamo wako kuhusu barua ya KKKT (Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania) umekuponza, ulikuwa na msimamo madhubuti na ulisimamia haki.”Hapo hapo mara tu baada ya ujumbe huo, Polepole aliibuka na kumjibu, Zitto Kabwe ni mzee wa kurukia treni kwa mbele.
“Mzee wa kurukia treni kwa mbele ushaanza, mbona unapenda ubashiri na vitendo vya kilozi. Rais hutenda impendezavyo kwa dhamana aliyopewa na Katiba. Sisi tuliohudumu kwenye Serikali na chama tunajua na kuheshimu, usijitatafutie huruma kwa mtu acha kupotosha hiyo si siasa safi.”

No comments :

Post a Comment