
Mwezeshaji
kutoka Sung Consultants Wakili, Harold Sungusia akiwasilisha mada juu
ya masuala ya uongozi kwenye mafunzo ya siku tano ya uongozi, utawala na
menejimenti jijini Dodoma. Mafunzo hayo yanaratibiwa na UNESCO kwa
ufadhili wa SDC. Mafunzo hayo yanajumuisha wamiliki na mameneja wa
redio za kijamii ambazo ni wanachama wa Mtandao wa vyombo vya habari
vya kijamii (TADIO).
Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji wakuu wa Jukwaa la Wahariri ambao waliwatembelea na kuongea nao.
SHIRIKA
la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeendesha
kongamano la siku tano lenye lengo la kufunza menejimenti, uongozi na
utawala kwa mtandao wa redio za jamii nchini (TADIO).
Kongamano hilo limefanyika Jijini Dodoma kuanzia Julai 17 – 21 .
Kwa mujibu wa UNESCO mafunzo hayo yamelenga kuimarisha mtandao huo.
Mafunzo
hayo yalifanywa kwa ajili ya watumishi muhimu wa radio hizo, bodi ya
mtandao, sekretarieti ya mtandao na wawakiklishi wa radio wanachama.
Lengo ni kusaidia redio hizo kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu.
Mafunzo
hayo yametokana na utafiti uliofanywa kuhusu menejimenti na uongozi wa
TADIO katika utekelezaji wake wa majumumu hasa kufuatia malengo ya uwapo
wa radio hizo.
UNESCO
ikisaidiwa na Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) kwa ufadhili wa
Empowering Local Radio kupitia tehama imetoa mafunzo hayo yenye lengo la
kuinua ubora wa kazi za redio hizo.
Mafunzo
hayo ni sehemu ya mradi unaowezesha redio 25 za kijamii zilizo
wanachama wa TADIO kuhakikisha kwamba wanatoa huduma zitakazowezesha
watu maskini, wanawake na wasichana kuwezeshwa kufanya maamuzi sahihi
kwa mambo yanayowagusa kwa kuzingatia taarifa wanazopata kupitia redio
hizo.
Pamoja
na mafunzo hayo UNESCO pia inajipanga kusaidia menejimenti ya TADIO na
miundombinu yake ili kuweza kutoa huduma bora, kutengenezwa majukwaa
elimu na mashirikiano.
TADIO inawanachama wa vituo vya habari na mikutano; vilabu vya waandishi wa habari na radio jamii.
Mtandao
huo unaendeshwa na Mkutano Mkuu ambao ndio wenye maamuzi katika masuala
yote ya uwajibikaji na utendaji wa sehemu mbaliombali za TADIO; Bodi na
sekretarieti inayoendesha shughuli za kila siku za mtandao.

No comments :
Post a Comment