Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja
wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu (kushoto) akimkabidhi Latifa
Mohammed Ngea kutoka Zanzibar (kulia) mfano wa hundi yenye thamani ya
shilingi milioni tatu mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa tuzo za
Umoja wa Mataifa za ubunifu akiwa miongoni mwa vijana watatu waliokuwa
wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja
vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es
Salaam yalifanyika.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja
wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu (kushoto) akimkabidhi Gracious
Fanuel kutoka Kilimanjaro (kulia) mfano wa hundi yenye thamani ya
shilingi milioni mbili mara baada ya kuibuka mshindi wa pili wa tuzo za
Umoja wa Mataifa za ubunifu akiwa miongoni mwa vijana watatu waliokuwa
wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja
vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es
Salaam yalifanyika.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja
wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu (kushoto) akimkabidhi Amos
Mtambala kutoka Dar es Salaam (kulia) mfano wa hundi yenye thamani ya
shilingi milioni moja mara baada ya kuibuka mshindi wa tatu wa tuzo za
Umoja wa Mataifa za ubunifu akiwa miongoni mwa vijana watatu waliokuwa
wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja
vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es
Salaam yalifanyika.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja
wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu akizungumza na waandishi wa
habari kuhusiana na tuzo za Umoja wa Mataifa za ubunifu kwa vijana
watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa
Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42
ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika.
Mshindi wa kwanza Latifa Mohammed
Ngea kutoka Zanzibar aliyebuni mfumo unaojiendesha wenyewe wa
umwagiliaji katika kilimo akizungumza na waandishi wa habari mara baada
ya kupokea tuzo ya Umoja wa Mataifa ya ubunifu akiwa miongoni mwa vijana
watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa
Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42
ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika.
Mshindi wa pili Gracious Fanuel
kutoka Kilimanjaro aliyebuni roboti kwa kutumia vifaa vinavyopatikana
majumbani akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea tuzo
ya Umoja wa Mataifa ya ubunifu akiwa miongoni mwa vijana watatu
waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa,
kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya
Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika.
Mshindi wa tatu Amos Mtambala
kutoka Dar es Salaam, ambaye anatumia kipaji chake cha sanaa kwa
shughuli za kijasiriamali akizungumza na waandishi wa habari mara baada
ya kupokea tuzo ya Umoja wa Mataifa ya ubunifu akiwa miongoni mwa vijana
watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa
Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42
ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika.
Mshindi wa tatu Amos Mtambala
kutoka Dar es Salaam, ambaye anatumia kipaji chake cha sanaa kwa
shughuli za kijasiriamali akizungumza na waandishi wa habari mara baada
ya kupokea tuzo ya Umoja wa Mataifa ya ubunifu akiwa miongoni mwa vijana
watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa
Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42
ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja
wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu akiwa katika picha ya pamoja na
mshindi wa kwanza Latifa Mohammed Ngea kutoka Zanzibar (katikati),
mshindi wa pili Gracious Fanuel kutoka Kilimanjaro (kushoto) pamoja na
mshindi wa tatu Amos Mtambala kutoka Dar es Salaam (kulia) huku wakiwa
wameshikilia hundi zao.
………….
Na Mwandishi wetu
LATIFA Mohammed Ngea kutoka
Zanzibar ameibuka kidedea katika tuzo za Umoja wa Mataifa za ubunifu na
kupata hundi ya shilingi milioni 3.
Latifa ni miongoni mwa vijana
watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la
Umoja wa
Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42
ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika.
Latifa alipata tuzo hiyo kwa kubuni mfumo unaojiendesha wenyewe wa umwagiliaji katika kilimo.
Mfumo huo unaojiendesha wa
umwagiliaji maji unaweza kutumia king’amuzi ili kubaini wapi pana unyevu
na wapi pakavu ili maji yaweze kupelekwa.
Tangu kuanza kwa maonesho hayo
takribani wiki sasa, wageni mbalimbali wamepata nafasi ya kuona ubunifu
wa vijana hao katika roboti, sanaa na kilimo.
Aidha walionesha ubunifu wao
unavyofanyakazi sanjari na kauli mbiu ya sabasaba mwaka huu inayosema
“Kukuza biashara kwa maendeleo ya viwanda”.
Baada ya wananchi kuwasikiliza
wabunifu wote watatu, wageni walipata fursa ya kupiga kura nani
waliamini alionyesha ubunifu bora zaidi, ndipo Latifa alipoibuka
mshindi.
Mbunifu mwingine alikuwa ni
Gracious Fanuel anayetoka mkoani Kilimanjaro alipata ushindi wa pili.
Huyu yeye alitengeneza roboti kwa kutumia vifaa vinavyopatikana
majumbani.
Roboti aliyotengeneza ni mfano wa
Mkono ambao unaweza kuendeshwa kwa simu ya mkononi na anatarajia kukuza
ubunifu wake ili ufikie hatua ya kuwa na mkanda wa uzalishaji bidhaa na
pia kusaidia watu wenye ulemavu.
Mbunifu mwingine ni Amos Mtambala,
kutoka Dar es Salaam, ambaye anatumia kipaji chake cha sanaa kwa
shughuli za kijasiriamali yeye alishika nafasi ya tatu. Amos alipata
mafunzo kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) na tangu hapo amekuwa
akipanua mtandao wake na kuwachukua zaidi ya vijana 100 ambao
hutengeneza kazi za sanaa na kuuza nchini na pia kimataifa.
Zaidi ya watu 500 katika Viwanja
vya Sabasaba na kupitia mitandao ya kijamii walipiga kura kwa kijana
yule wanayeamini aliandaa ubunifu bora zaidi.
Mshindi wa kwanza alipata shilingi milioni 3 huku mshindi wa pili akipata shilingi milioni 2 na wa tatu shilingi milioni 1.
Wabunifu hao watatu walikuwa
miongoni mwa vijana 100 kutoka nchi nzima walioshinda ili kuonyesha
ubunifu wao katika banda la UN. Hawa walichaguliwa kwa umakini ili
kuendana na ujumbe wa mwaka huu wa Sabasaba, ambao ni Kukuza Biashara
kwa Maendeleo ya Viwanda.
Akizungumza katika banda la
maonyesho la Umoja wa Mataifa wakati wa kutangaza washindi, Mtaalamu wa
Mawasiliano wa UN, Bi. Hoyce Temu, aliwapongeza vijana ambao kwa kuwa na
ndoto ya serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha kwamba azma ya
maendeleo ya viwanda inatimia.
Banda la maonyesho la UN ambalo
Jumatano lilitangazwa kushika nafasi ya kwanza katika eneo la Utoaji
Taarifa, Machapisho, Habari na Mawasiliano kwa jamii ni moja ya mabanda
yaliyokuwa na pilika nyingi.
Kupatikana kwa Tuzo hiyo
iliyokabidhiwa na Waziri Mkuu, Mh. Kassim Majaliwa, wakati wa ufunguzi
wa Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam kumetokana
na mkazo wa banda hilo mwaka huu la kutoa taarifa za matokeo na
ushaiishaji wa UN katika Ubunifu kwa ajili ya Maendeleo Endelevu.
Umoja wa Mataifa Tanzania
umeshinda nafasi ya kwanza katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya
Dar es Salaam mara kadhaa tangu UN ilipoanza kushiriki, kwani imeshiriki
mara 8 mfululizo. Umoja wa Mataifa una nia ya kuendelea kushiriki ili
kuwafikia watu wengi zaidi walio nje ya mfumo rasmi katika muktadha wa
Sabasaba na Nanenane.
Kikosi Kazi cha Mawasiliano cha
Umoja wa Mataifa (UNCG), ambacho ni kundi linalojumuisha maofisa wote wa
Mawasiliano kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi
nchini Tanzania, lina wajibu wa kubuni na kusimamia maandalizi ya banda
la maonyesho.
No comments :
Post a Comment