Kamishna
wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya
(katikati) akitoa maagizo kwa uongozi wa Kiwanda cha Manyara Sugar Company
Limited kuhusu kutoa takwimu sahihi uzalishaji sukari wakati alipofanya ziara
ya kikazi kusikiliza changamoto za Wafanyabiashara.
NA RACHEL MKUNDAI, MANYARA
MAMLAKA ya
Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara wenye viwanda vya kutengeneza
mali ghafi za kutengenezea pombe kali kutoa tawimu sahihi ya kiasi kinachozalishwa
na mahali inapouzwa ili serikali iweze kukusanya kodi yake stahiki kupitia
pombe kali.
Hayo
yamesemwa na Kamishna waKodi za Ndani wa TRA Bw Elijah Mwandumbya mara baada ya
kutembelea kiwanda cha kutengeneza sukari cha Manyara Sugar Company Limited
kilichopo mkoani Manyara na kuongeza kuwa takwimu hizo zitawezesha TRA
kufuatilia kwa karibu na kupata takwimu sahihi za kikodi na kuongeza makusanyo
ya mapato.
“Tunafahamu
kwamba “Molasis” au mali ghafi inayotokana na zao la miwa baada ya
kutengeneza sukari ni bidhaa inayotumika kutengenezea pombe kali na hivyo
takwimu zitatuwezesha kufuatilia wafanyabiashara wanaonunua bidhaa hiyo na
kutengenezea pombe kali ili nasi tukadai kodi yetu na kodi hiyo ilete tija kwa
taifa”, amesema Bw. Mwandumbya
Naye Mkuu
wa mkoa wa Manyara Bw. Alexander Mnyeti amesema mkoa una mkakati wa kuongeza
viwanda vingi vikubwa na vidogo ili viweze kuleta tija kwa mkoa kwa kuongeza
ajira na pato la taifa kwa ujumla.
“Tunataka
kuongeza viwanda vingi katika mkoa wetu ili serikali iweze kupata kodi zaidi na
kuongeza mapato kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wetu”, amesema Bw. Mnyeti.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa kiwanda cha sukari cha Manyara Sugar Company Limited, Bw.
Pratap Sisudya ameshukuru ujio wa Kamishna wa kodi za ndani na kuahidi
kushirikiana na TRA kuhakikisha kuwa wanalipa kodi zote kwa wakati pamoja na
kutoa takwimu sahihi za uzalishaji wa kiwanda.
“Ni wajibu
wetu kutoa taarifa zahihi kwa TRA pamoja na kulipakodi stahiki kwa wakati
ambapo kwa mwaka 2017/2018 tumelipa kodi kwa serikali takribani Shilingi
bilioni 1”, alisema Bw. Sisudya.
Kiwanda
cha Manyara Sugar Company kinazalisha zaidi ya tani 4,000 za sukari kwa mwaka
na kina mashamba ya miwa ekari 1,600 na kutoa ajira za muda kwa watu 350 hadi
400 kwa siku.
Kamishna
wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (wa
pili kulia) akiwa ameongozana na uongozi wa Kiwanda cha Manyara Sugar Company
Limited kuelekea katika eneo la uzalishaji sukari wakati alipofanya ziara ya
kikazi kusikiliza changamoto za Wafanyabiashara.
Kamishna
wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya
(kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Kiwanda cha Manyara Sugar Company Limited,
Bw. Pratap Sisudya wakati
alipofanya ziara ya kikazi kusikiliza changamoto za Wafanyabiashara.
Mkurugenzi
wa Kiwanda cha Manyara Sugar Company Limited, Bw. Pratap Sisudya (katikati) akimweleza
Kamishna
wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (wa
pili kulia) moja ya mtambo utumikao kuzalisha sukari wakati alipofanya ziara ya
kikazi kusikiliza changamoto za Wafanyabiashara.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA)
No comments :
Post a Comment