Monday, July 30, 2018

Tanzania yaingia kwenye historia ya dunia kwa kuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki kuteuliwa mjumbe wa UNBoA


AS1
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za Serikali  (CAG) Profesa Juma Assad akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa Dege wa JINA ukumbi wa VIP mara baada ya kurejea kutoka Marekani ambako alishiriki  mikutano miwili ya kimataifa iliyojadili na kuweka malengo na maazimio ya Umoja wa Mataifa katika masuala ya udhibiti na ukaguzi wa hesabu za serikali kushoto ni Idrisa Msuya  Kaimu Msaidizi wa Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Serikali.
AS02
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu  za Serikali (CAG) Profesa Juma Assad akifafanua jambo katika mkutano huo.
AS2
Baadhi ya wakurugenzi na wakuu wa vitengo ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa  Hesabu za Serikali Serikali.
AS3
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Profesa Juma Assad wakati akizungumza.
…………………………………………………………………………….
Na John Bukuku
MKAGUZI na mdhibiti wa Hesabu za Serikali Profesa  Mussa  Assad Amesema kuwa Tanzania imeingia kwenye historia ya dunia kwa kuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki na
kati kuteuliwa kuwa mjumbe wa UNBoA na kwa Afrika Tanzania ni nchi ya tatu kuwa Mjumbe wa UNBoA.
Nchi zingine kwa Afrika ambazo  zimewahi kuwa mjumbe wa UNBoA ni nchi ya Ghana pamoja na nchi ya Afrika kusini tu.
Profesa Assad amesema hayo jana jijini Dar es Salaam leo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya kutua uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere akitokea nchini Marekani.
Assad amerejea nchi leo kutoka Marekani ambapo alihudhuria mikutano miwili ya kimataifa iliyofanyika kwa vipindi tofauti  kwa mwezi julai  2018 jijini NewYork nchini Marekani ambapo pia mkutano wa kwanza  ulijadili kuweka Malengo.
Ametolea  ufafanuzi malengo hayo kuwa na maazimio yaliyokubalika kwenye mkutano huo profesa  Assad alisema malengo mengi yanatekelezeka isipokuwa machache huku akitolea mfano lengo la 16  linalosema kuzingatia Aman na kufanya Taasisi Imara na zenye Nguvu .
Kuhusu ushiriki wa Tanzania kama mjumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa Amesema kikao cha 72  cha mwisho kwa nchi ya Tanzania kuhudhuria kama mjumbe wa UNBoA.
Pia amesema kwa nafasi yake ya Ujumbe wa UNBoA Tanzania ilikuwa pia mjumbe wa Jopo la wakaguzi wa Nje wa Umoja wa Mataifa . 
  Amesema  mbali na kumaliza muda wake ambao umedumu kwa miaka sita lakini pia itabaki kuwa Mjumbe Mwangalizi ” (Obsever Member) kwenye jopo la wakaguzi wa Nje wa umoja wa Mataifa kwa kipindi cha miaka tatu mfululizo tangu ing’atuke kwenye nafasi ya Ujumbe wa UNBoA.
Changamoto nyingine waliyokutana nayo wakati wa ukaguzi wa UN ilikuwa ni uwezo wa kukagua mifumo ya kielektroniki ambapo amefafanua kuwa kuwepo kwa changamoto hiyo kulisababisha Ofisi yake kujipanga vizuri ikiwemo kuendesha mafunzo mbalimbali ili kuongezea wakaguzi wake uwezo.
“Tumejitahidi sana kuhakikisha tunalinda heshima ya serikali yetu kwa kuhakikisha wakaguzi wetu wanaujuzi na utalamu unaokubalika katika viwango vya kimataifa.”alisema Assad
Nakwambai ingekuwa jambo la aibu sana kama ripoti zetu zingekataliwa na Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa au kamati za usimamizi fedha na utawala za UN .”alisisitiza
Ameongeza kuwa katika kipindi chote cha miaka sita ripoti zetu zote zimekidhi ubora unaohitajika na hivyo kukubaliwa kuidhinishwa na Bodi ya Ukaguzi ya UN nakwamba kwasasa Tanzania inapomaliza muda wake wanajivunia wakaguzi bora zaidi wa mifumo ya kielektroniki na ujuzi katika maeneo mbalimbali ,ambapo pia ujuzi walioupata huko watautumia hapa nyumbani.
  Assad amesema licha ya Tanzania kumaliza muda wake wa ujumbe wa Bodi  ya Ukaguzi  ya UN bado Tanzania inapaswa kusimamia ripoti zake na kuzitolea ufafanuzi kwenye kamati maalum za usimamizi za UN wakati wote wa ripoti hizo zinapojadiliwa kwenye kamati hizo.
Amemaliza kwa kusema watumishi kutoka ofisi ya Taifa ya Ukaguzi zaidi ya 200 wamepata fursa ya kukagua miradi ya UN inayotekelezwa katika nchi zaidi ya 51 duniani.

No comments :

Post a Comment