Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiteta jambo na Waziri wa
Madini Mhe. Angellah Kairuki wakati wa mkutano wa hadhara katika Uwanja
wa Sabasaba wilaya ya Chunya ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara ya Makamu
wa Rais mkoani Mbeya. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu
Waziri wa Kilimo Dkt. Mary Mwanjwelwa mara baada ya kumalizika kwa kikao
cha majumuisho ya ziara yake katika Ukumbi wa Mkapa mkoani Mbeya.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa
Chunya kwenye uwanja wa Sabasaba ikiwa ni siku ya kuhitimisha ziara yake
mkoani Mbeya. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amehitimisha
ziara yake ya siku 6
mkoani Mbeya ambapo ameupongeza mkoa huo kwa kutunza mazingira.
“Naomba sana ule utaratibu wa Machifu kusimamia Mazingira uendelee”
alisema Makamu wa Rais.
Katika ziara hiyo ya siku 6 ya kukagua na
kuhamasisha shughuli mbali mbali za kimaendeleo, Makamu wa Rais amesema
Uchumi wa Viwanda unaunganishwa na miundombinu hivyo Mbeya imekidhi
vigezo kwani pamoja na kuwa na barabara nzuri pia ina meli tatu ambazo
kati ya hizo mbili ni za mizigo na moja ya abiria na mizigo.
Mapema leo Makamu wa Rais alifanya ziara
katika wilaya ya Chunya na kujionea Viwanda vinavyojishughulisha na
uchenjuaji madini ya dhahabu ambapo alitoa Maagizo kwa Uongozi wa Mkoa,
Halmashauri pamoja na Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) kuhakikisha
viwanda vya uchenjuaji madini vina vibali vyote muhimu kabla ya
kupatiwa leseni.
Wakati huo huo Waziri wa Madini Mhe.
Angellah Kairuki amesema Serikali imeweka zuio la usafirishaji wa Kaboni
ambazo zinabeba madini ya dhahabu kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa
mwingine kwa lengo kubwa la kuweka ulinzi na usalama na kusema
kitakachotoka kutoka mmoja kwenda mwingine ni dhahabu ambayo
imeshachenjuliwa.
Waziri Kairuki amesema kuwa Wote wenye
leseni za Uchimbaji na hawajaendeleza maeneo yao watafutiwa leseni hizo
na kupatiwa watu wengine.
Mwisho, Makamu wa Rais alihitimisha ziara
yake kwa kufanya kikao cha majumuisho na Uongozi wa Mkoa wa Mbeya ambapo
aliupongeza kwa kuwa na vituo vya afya 316, chakula cha kutosha lakini
pia alisisitiza Uongozi huo wa mkoa kufanya jitihada za kutoa elimu ya
lishe kwa jamii kwani kiwango cha udumavu kwa watoto ni kikubwa.
No comments :
Post a Comment