Kijana
wa Chipukizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ikungi, Amina
Abdallah akimvika skafu Katibu Mkuu wa CCM, Dk.Bashiru Ali baada ya
kuwasili Wilaya ya Ikungi katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani
Singida leo hii. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi,
Mika Tano Likapakapa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Hassan
Kilimba.
Kikundi cha Utamaduni cha Liti kikitoa burudani wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu, Dk.Bashiru Ali.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Singida, Hassan Kilimba (kulia), akimuelekeza jambo
Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ali baada ya kuwasili wilayani Ikungi.
Dk.Bashiri akisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili wilayani Ikungi.
Dk. Bashiru akiwasalimia wana CCM.
Dk. Bashiru akisaini katika kitabu cha wageni.
Makada wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kupokea Katibu Mkuu.
Mkutano ukiendelea.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Makada wa CCM wakiimba wimbo wa Taifa.
Makada wa CCM wakijitambulisha kwa Katibu Mkuu.
Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu Mzee Yusuph Makamba akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Singida, Diana Chilolo.
Katibu
Mkuu wa CCM Mstaafu Mzee Yusuf Makamba akisalimiana na Katibu Mkuu wa
CCM, Dk.Bashiru Ali. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida,
Hassan Kilimba.
| Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Jimbo hilo, mbele ya Katibu Mkuu. |
Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu Mzee Yusuph Makamba , akizungumza kwenye mkutano wa kumpokea Katibu Mkuu mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, .Miraji Jumanne Mtaturu, akitoa taarifa ya maendeleo kwa Katibu Mkuu.
Katibu Mkuu wa CCM, Dk.Bashiru Ali akipitia taarifa mbalimbali za maendeleo.
Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mussa Sunja, akitoa taarifa.
Katibu
Mkuu wa CCM, Dk.Bashiru Ali na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida,
Hassan Kilimba wakionesha silaha za jadi baada ya Wazee wa Mkoa wa
Singida kumsimika rasmi.
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akimsikiliza kwa
umakini Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe Godwin Gondwe wakati wa ziara
yake
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amemsimamisha
Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Wilaya Korogwe Mji Joseph Mcharo kwa
kutumia force accout kwenye mradi wa zaidi ya Milioni 700 bila ya kibali
toka Wizara hiyo.
Agizo la kusimamishwa kwa Mhandisi huyo
alilitoa jana wakati akikagua mradi miwili ya maji ya Mtonga ambao
umetumia zaidi ya milioni 700 na msambiazi ambao umetumia zaidi ya
milioni 600 ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya mkoa wa Tanga ambayo
ilianza juzi wilayani Handeni.
Alisema mradi huo ulitakiwa
kutumia kiasi cha shilingi Milioni 500 na wataalamu hao wakaubadilisha
na kuufanya uwe wa milioni 700 ingawa bado unaendelea kusuasua jambo
ambalo linaonyesha ubadhirifu wa fedha za Serikali
Akiwa kwenye
mradi wa Mtonga baada ya kumalizika kuukagua alitilia mashaka na ndipo
alipoamuru mhandisi huyo kumpatia maelezo ya kina kuhusiana na mradi huo
lakini pia hakuridhika na maelezo hayo na kuagiza kuwa atapeleka
wataalamu kutoka wizara ili kuweza kuhakiki thamani ya fedha na ubora
mrai huo.
“Kwa kweli mimi hapa sijaridhika na utekelezaji wa
mradi huu unaonekana upo chini ya kiwango na ucheleweshwaji huku
wananchi wakiendelea kupata tabu hivyo nitatuma wataalamu kutoka
wizarani waje kuhakiki mradi huo”Alisema
Baada ya ukaguzi wa
mradi huo Naibu Waziri huyo aliambatana na viongozi mbalimbali wa
halmashauri ya Korogwe mji kuelekea kwenye mradi wa Msambiazi ambako
kunajengwa tenki kubwa la mradi utakaosambaza maji kwa wananchi.
Akiwa
huku ndipo alipomuuliza mhandisi gharama za mradi ambapo alisema zaidi
ya milioni 600 zimetumika kwa kutumia mfumo wa mkandarasi na kupelekea
mradi huo kufikia kwenye hatua za mwisho jambo ambalo limeibua maswali
mengi kwa Naibu Waziri na kuamua kuchukua uamuzi huo.
“Ndugu
zangu haiwezekani mradi wa zaidi ya milioni 700 kutumia force account
kinyume na taratibu za wizara huku mradi wa milioni 600 ukitekelezwa
kupitia mkandarasi ni wazi kwamba kuna ubadhirifu unaendelea hapa na
mimi sitakubali”Alisema.
Baada ya maelezo hayo Naibu Waziri
aliamua kumsimamisha mkandarasi huyo kwa kigezo miradi inayotumia chini
ya milioni 200 ndio inapaswa kutumia force acounti tofauti na
alivyofanya mhandisi huyo huku akimdanganya kwamba anakibali kutoka
wizarani.
Awali akijib u hoja za Naibu Waziri huyo Mhandisi wa
Maji Halmashauri ya Korogwe Mji Joseph Mcharo alidai anakibali cha
wizara kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa mtonga kutumia force acounti
ndipo Naibu Waziri huyo alipoamua kupiga simu wizara kupata
ufafanuzi.
Naye
kwa upande wake Mkurugenzi wa Halamshauri ya Korogwe Mji Jumanne Shauri
alionekana kushindwa kujibu maswali ya Naibu Waziri jambo ambalo
liliibuka mabishoni baina yao kabla ya Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe
Godwin Gondwe kumtaka Mkurugenzi akiri mapungufu yaliyojitokeza kwenye
mradi huo.
Mradi wa Mtonga ambao Naibu Waziri Aweso aliitulia
mashaka ni wa kusambaza tenki,mabomba na sehemu maalumu kwa ajili ya
mtambo wa kutibia na kusafisha maji eneo la mradi husika
No comments :
Post a Comment