Monday, July 23, 2018

“HALIPENDWI SHIRIKA, HAPA PESA TU”: RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU WAKATI AKIPOKEA GAWIO LA SH. BILIONI 723.61 KUTOKA KWA WANAHISA WAKE


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara   katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 23, 2018
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo Julai 23 2018, amepokea mfano wa hundi zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 723.61, ikiwa ni gawio kutoka Mashirika, Taasisi na Kampuni 40 ambazo Serikali ina hisa.
Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere(JNICC) jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais  Magufuli, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango alisema, fedha hizo ni asilimia 15 ya ,mapato ghafi kutoka, Taasisi, Mashirika ya Umma na Makampuni na kuchangia kwenye mfuko mkuu wa serikali.
Akizunguzma kwenye hafla hiyo, Rais Magufuli alipongeza Taaisi, Mashirika na Kampuni ambazo zimefanikiwa kuwasilisha gawiwo la serikali.
Hata hivyo Rais alisema Serikali imewekeza zaidi ya Shilingi Trilioni 49 na kwamba haiwezekani ipate gawio la Shilinhgi Bilioni 736, hivyo amemuagiza Msajili wa Hazina ambaye ndiye anayesimamia taasisi, Mashirika na Makampuni yenye ubia na Serikali kuhakikisha wanatoa gawiwo.
na yatakayoshindwa uongozi wake ubadilishwe au yafutwe. “Hapa pesa kwanza halipendwi shirika inapendwa pesa” Alisema. Rais Mahifuli.
Alisema, zipo njia nyingi za kukusanya mapato ya serikali na mojawapo ni hii ya kupoeka gawiwo kutoka Mashirika, Taasisi na Makampuni ambayo Serikali ina hisa zake.
“Huwezi kuendesha nchi kwa kutegemea makusanyo ya kodi pekee, na tulipofanya utafiti kwanini serikali haipati mapato yake kutoka kwenye uwekezaji iliyoufanya kwenye mashirika, Taasisi na Makampuni, tulibaini kuwa ni uongozi mbovu, na kukithiri kwa rushwa.” Alibainisha Rais Magufuli.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais Magufuli, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango alisema, “Makampuni, Taasisi na Mashirika ambayo hayajawasilisha gawio, wajitathmini, ikiwa ni pamoja na wawekezaji ambapo bado hawajatimiza malipo wafanye hivyo mara moja.” Alisema Dkt. Mpango
Alitaja Mashirika, Taasisi ambazo zimevuka lengo la ukusanyaji wa mapato waliojiwekea kuwa ni pamoja na Ngorongoro Conservation Area, ambao walilenga kutoa Bilioni 13.24 lakini wakaongeza hadi Shilingi Bilioni 22.35 na Taasisi nyingine ni
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), amabayo lengo ilikuwa ni kupeleka gawiwo la Shilingi Bilioni 30.69, lakini wamepeleka Shilingi Bilioni 59.89 wakati TANAPA walijiwekea lengo la kuleta Shilingi Bilioni 30.77 lakini wamepeleka Shilingi Bilioni 34.74
Hata hivyo bado kuna mashirika 158 bado yanategemea ruzuku kutoka serikalini huku makampuni 48 yameshindwa kutoa gawio
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya TIPER Profesa Abdulkarim Mruma  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 23, 2018  

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Bw. Edwin Rutageruka
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mfuko wa Misitu Tanzania akiwa na Katibu Dkt. Tuli Salum Msuya  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 23, 2018  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na (EWURA) Maji Profesa Jamidu Kamika akiwa na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa  EWURA Bw. Nzinyangwa Mchani  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 23, 2018  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekliti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Profesa Rutasitara akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 23, 2018  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Balozi Ben Moses akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa TFDA Bi. Agnes Kijo   katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 23, 2018


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa Shirika la Viwango (TBS)  Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko akiwa na  Mkuruigenzi wa TBS Profesa Egird Mubofu  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 23, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari  Profesa Ignas Rubaratuka aliye pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi Deusdedit Kakoko  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 23, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa  Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Bonde la Ngorongoro Profesa Abiud Lucas Kaswamila akiwa a Mhifadhi Mkuu wa  Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Dkt. Freddy Manongi  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 23, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akikabidhi Cheti cha kutambua kuvuka malengo ya gawio  kwa  Mwenyekiti wa Bodi Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA)  Dkt. Jonas Kilimbe akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kulaba  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 23, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu wakipata picha ta pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumua ya Bunge ya Uwekezaji wa Mtaji wa Umma baada ya kupokea magawio kutoka katika taasisi, mashirika na Makampuni ya Umma katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 23, 2018,(PICHA NA IKULU)

No comments :

Post a Comment