Friday, July 20, 2018

DKT. NDUGULILE AZINDUA MPANGO WA MAFUNZO KWA WANAFUNZI NA WALIMU KUZUIA UKATILI SHULENI


  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, JInsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwisenge iliyopo Musoma Mkoani Mara mara baada ya kuwasilia kuzindua mpango wa mafunzo kwa wanafunzi na walimu ili kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia shuleni.

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza  na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwisenge iliyopo Musoma Mkoani Mara kutofanyiana vitendo vya ukatili na kutoa taarifa ya vitendo hivyo shuleni kabla ya kuzindua mpango wa mafunzo kwa wanafunzi na walimu ili kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia shuleni.

  Mkuu wa Wilaya ya Musoma Bw.Vicent Naano akielezea mikakati ya Wilaya katika  kupambana na wale wote watakaosababisha au kuwafanyia wanawake na watoto vitendo vya ukatili katika uzinduzi wa mpango wa mafunzo kwa wanafunzi na walimu ili kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia shuleni.

  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa USAID  akielezea mikakati ya Serikali ya Marekani kushirikiana na  Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na mimba na ndoa za utotoni katika uzinduzi wa mpango wa mafunzo kwa wanafunzi na walimu ili kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia shuleni.

  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwisenge iliyopo Wilaya ya Musoma Mkoani Mara wakisikiliza nasaha kutoka kwa viongozi mbalimbali wakati wa  uzinduzi wa mpango wa mafunzo kwa wanafunzi na walimu ili kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia shuleni.

 Baadhi ya wazazi na wanafunzi
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwisenge iliyopo Wilaya ya Musoma Mkoani Mara wakisikiliza nasaha kutoka kwa viongozi mbalimbali wakati wa  uzinduzi wa mpango wa mafunzo kwa wanafunzi na walimu ili kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia shuleni.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, JInsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizindua Mpango wa mafunzo kwa wanafunzi na walimu ili kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia shuleni katika Shule ya Sekondari Mwisenge iliyopo Wilaya ya Musoma mkoani Mara.(PICHA NA  WAMJW)
NA MWANDISHI WETU- MARA
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, JInsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amezindua mpango wa mafunzo kwa wanafunzi na walimu ili kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia shuleni
Akizungumza katika uzunduzi wa mafunzo hayo uliofanyika katika Shule ya Sekondari Mwisenge Dkt. Ndugulile amesema kuwa vitendo vya Ukatili wa kijinsia hususani ukatili dhidi ya wanawake na watoto umeendelea kuwepo chini na takwimu zikionesha mkoa wa Mara ukiwa na asilimia 32 ya vitendo hivyo.
Ameongeza kuwa mimba na ndoa za utotoni bado ni tatizo kubwa ambapo mkoa wa Mara ni wa tano kitaifa kwa kuwa na asilimia 37.
“Serikali imeandaa Mpango wa kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa mwaka 2017/18-2021/22 na moja kati ya msisitizo katika mpango huu ni kutokomeza ukatili wa kijinsia shuleni” alisisitiza Dkt. Ndugulile
Aidha Dkt. Ndugulile amekemea mahusiano ya kingono yaliyopo baina ya walimu na wanafunzi na kuwataka wanafunzi kuacha kufanyiana vitendo vya ukatili na kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt.Vicent Naano amesema kuwa wataendelea kupambana na wale wote watakaosababisha au kuwafanyia wanawake na watoto vitendo vya ukatili.
Pia Mwakilishi wa Mkurugenzi wa USAID Bi.Christina Djondo ameihakikishia Serikali ya Tanzania kuendelea kushirikiana nayo katika mapambano dhidi ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na mimba na ndoa za utotoni.
Mpango huu wa mafunzo kwa walimu na wanafunzi utawafikia walimu 1,300 na wanafunzi 26,000.

No comments :

Post a Comment