Balozi
wa Tanzania Visiwani Komoro Mhe. Sylvester Mabumba alikutana na kufanya
mazungumzo na uongozi mpya wa Diaspora ya Watanzania waishio Komoro
(TADICO) tarehe 23 Julai 2018. Viongozi hao wapya walifika ofisi za Ubalozi kwa ajili ya kujitambulisha ambapo miongoni mwa mambo waliyojadili ni pamoja na kutoa
ahadi ya kuinua Diaspora ya Watanzania waishio Comoro ambapo kwa muda
mrefu Diaspora hiyo imeonekana kuwa nyuma kimaendeleo ikilinganishwa na
Diaspora za nchi nyingine.
Kwa
upande wake Mhe. Balozi Mabumba alichukua fursa hiyo kuwapongeza
viongozi hao wapya waliochaguliwa pamoja na kuwatakia kila la kheri
katika nafasi zao hizo mpya walizoaminiwa na Watanzania wenzao. Aidha,
Mhe. Mabumba alisisitiza juu ya umuhimu wa wanachama kulipa michango ya
uanachama na vilevile kuwaomba viongozi kuwa wasimamizi wazuri wa
matumizi ya fedha za wanachama hao.
Katika
hatua za kuhuisha chama hicho wajumbe walishauriwa pia kuwa wabunifu
katika mikakati yao na vilevile waangalie njia gani bora za kuibua
vyanzo vipya vya mapato badala ya kutegemea michango ya wanachama pekee.
Pia Balozi Mabumba aliwahimiza viongozi hao kutosahau kuwekeza nyumbani
na vilevile kuchangamkia fursa za biashara ambazo zinapatikana Tanzania
na kuzitangaza Visiwani humo.
 |
Balozi
wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Balozi
Sylivester Mabumba (kati) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa
Ubalozi na viongozi wa Diaspora visiwani Comoro. Kutoka Kushoto ni Bw..
Hussein Banoga, Makamu Mwenyekiti; Bw..
Khamis Salum, Mweka Hazina; Bw.. Thabit Khamis, Afisa Ubalozi; Bw..
Fikiri
Salum, Katibu Mkuu; Bw. Salum Ali, Mwenyekiti; Bw.
Fuastine, Bw. Isakwisa na Bw. Mudrick Soragha.
|
 |
| Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja. |
No comments :
Post a Comment