Friday, June 29, 2018

WAJIBU WA WAAJIRI KUWASILISHA MICHANGO MIFUKO YA PENSHENI


Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akimkabidhi ngao Meneja wa Breez Beach Club, Jacob Myaya wakati wa utoaji zawadi kwa mashirika bora yanayochangia michango ya wanachama wa mfuko wa ZSSF. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya ZSSF, Dk. Suleiman Rashid.
 
 
CHRISTIAN GAYA,
MIFUMO ya hifadhi ya jamii ambayo ni ya lazima kisheria ambayo wafanyakazi pamoja na mwajiri wanachangia pamoja na kupeleka michango kwenye chombo cha mfuko wa pensheni, ingawa inatoa
mipango mengine ya hifadhi ya jamii kwa mfumo wa hiari kama mafao ya ziada.
Jukumu la kuhakikisha michango ya wanachama inalipwa kwa wakati muafaka ni la mwajiri mwenyewe na wafanyakazi wake. Hata hivyo ili kuhakikisha waajiri na wafanyakazi wanajiandikisha na kulipa michango kwa wakati, inatakiwa wakaguzi kufanya kaguzi kwa waajiri kila mara inapobidi. 
Kila mwajiriwa ambaye ni mwanachama wa mifuko hii anayo haki ya kufuatilia katika ofisi za mfuko zilizoko karibu naye ili kuhakikisha kama mwajiri wake anatimiza wajibu wa kuwasilisha michango hiyo.
Viongozi wa chama cha wafanyakazi kazini wana wajibu pia wa kumkumbusha mwajiri mara kwa mara ya kuhakikisha ya kuwa anawasilisha michango sahihi ya kila mfanyakazi yaani mwanachama kwa wakati muafaka na kupata taarifa ya michango yake anayokatwa kama haki yake kisheria.
Pamoja na kuwa na wakaguzi ambao kisheria wamepewa nguvu kubwa kisheria kuingia mahali popote kuchunguza, kuwaelemisha, kuandikisha waajiri kuwa wachangiaji wa mifuko ya pensheni, kukusanya michango na kuwakumbusha wajibu waajiri wa kukata kutoka katika mishahara ya wafanyakazi wao na kupeleka michango hiyo kwenye mfuko husika kwa muda unaotakiwa kila baada ya mwezi mmoja.
Idadi ya waajiri ambao hawalipi michango ya wanachama wa mifuko hii ya pensheni kila siku inazidi kuongezeka.
 
Kwa maana ya kwamba waajiri wamepewa kuchelewesha michango muda wa mwezi mmoja. Na wakichelewesha zaidi ya mwezi huo mmoja michango hiyo inavutia adhabu karibu ya asilimia tano ya kila mchango uliotakiwa kupelekwa kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii.
Si hivyo tu, wamepewa mamlaka ya kumfungulia mashitaka mwajiri anayewazuia kufanya kazi zao za ukaguzi. Na inapobidi kufungua na kuendesha kesi mahakamani wao wenyewe wakaguzi.
Sheria inasema wanaweza kufunguliwa kesi za madai au za jinai pale mazingira yanaporuhusu ya kuweza kuokoa michango ya wanachama.
Sheria inaruhusu kukamata na kuuza mali inayohamishika au isiyohamishaka au kumfilisi mwajiri ili kupata michango ya wafanyakazi wake ambao ni wanachama wa mifuko ya pensheni. 
Sheria baadhi ya mifuko hii ya pensheni kama siyo yote inasema hata hivyo mwajiri atakapopatikana na hatia anaweza kutozwa faini na kufungwa kwa miaka mitatu jela.
Lakini kwa upande mwingine wa shilingi mifuko huwachukuliwa hawa waajiri kama wateja wao na kwa upande wa mila na desturi ya ushindani mteja ndiye mfalme kwa hiyo lazima umuhudumie ipasavyo kwa kutoa huduma bora na ya hali ya juu kuliko mshindani wake.
Lakini cha kusikitisha ni kwamba hata ile asilimia 10 au 5 mwajiri aliyokata kwenye mshahara wa mfanyakazi nayo unakuta  anashidwa kulipa kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii. 
Christian Gaya ni mwanzilishi wa Kituo cha HakiPensheni Tanzania, mshauri na mtaalamu wa masuala ya pensheni. Kwa maelezo zaidi wasiliana kwa: gayagmc@yahoo.com unaweza kutembelea tovuti hakipensheni monitor online na hakipensheni blog Simu namba +255 655 13 13 41 info@hakipensheni.co.tz

No comments :

Post a Comment