Video: Majaliwa apiga marufuku gari za serikali kulala nyumbani kwa mtu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa agizo
zito kwa watumsihi wa Halmashauri ambapo amesema kuanzia leo gari zote
za Serikali baada ya muda wa kazi zinatakiwa kurudi halmashauri na kumpa
kazi mkurugenzi kusimamia suala hilo.
Pia amepiga marufuku kwa mtumishi yeyote wa serikali anayetumia gari za serikali kulaza gari hiyo nyumbani kwake.
”Kuanzua leo gari zote za sereikali zote, zote baada ya miuda wa
kazio ziwe kjwenye yard ya mwandisi kama kuna gari itakuwa nje ya kituo
mkurugenzi atakuwa anajua na ni kwa kazi maalumu ya serikali na
haturuhusu mtu yeyote kukaa na gari ya serikali nyumabni kwake” Amesema
Majaliwa.
Waziri Mkuu, ameongea hayo leo pindi alipokuwa akihutubia jijini
Dodoma wilayani Bahi ambapo pia ameagiza watumishi wote wanaoishi nje ya
eneo la kazi wawe wamehamia.
Amwaagiza
watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma wanaoishi nje
ya eneo lao la kazi wawe wamehamia ifikapo July 30, mwaka huu.
No comments :
Post a Comment