Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi
anasikitika kutangaza kifo cha Daktari bingwa wa usingizi kwa watoto na
wagonjwa mahututi Onesmo Mhewa kilichotokea jana jioni tarehe
02/05/2018.
Mwili
wa Marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha
Hospitali ya Taifa Muhimbili na unatarajiwa kusafirishwa kesho tarehe
04/05/2018 kwenda katika kijiji cha...
Nzihi kilichopo Iringa vijijini kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika tarehe 05/05/2018.
Heshima
za mwisho zitatolewa kesho tarehe 4/5/2018 katika ukumbi wa kufundishia
uliopo chumba cha kuhifadhia maiti Muhimbili kuanzia saa 2 asubuhi hadi
saa 3 na baadaye nyumbani kwa kaka wa Marehemu kuanzia saa 6 mchana.
Kwa namna ya kipekee Prof. Janabi anatoa pole kwa familia ya Marehemu, Wafanyakazi wote, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wote walioguswa na msiba huu.
Msiba uko nyumbani kwa kaka wa marehemu Ndugu Lumumba Mhewa mtaa wa Mivumoni Madale.
“Bwana Ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe”.
No comments :
Post a Comment