Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndegulile akikata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara
ya Mkemia Mkuu wa Serikali leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu ambae alimwakilisha Katibu Mkuu
wa Wizara ya Afya Dkt. Otilie Gowelle.kulia ni Mwenyekiti wa bodi hiyo
Dkt Esther Jason.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndegulile akimkabidhi
Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Esther Jason mwongozo wa Bodi Tendaji ya Kwanza
ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Wapili kushoto ni
Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu ambae alimwakilisha Katibu Mkuu
wa Wizara ya Afya Dkt. Otilie Gowelle.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndegulile akimkabidhi
vitendea kazi Mkemia Mkuu wa Serikali Fidelice Mafumiko wakati wa
uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu
wa Serikali leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkemia Mkuu
wa Serikali Dkt. Esther akiongea akitoa neno mbele ya viongozi wa
Serikali na Waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya
Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndegulileakisisitiza jambo
mbele ya Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mku na
viongozi wengine wa Srikali wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza
ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu.
Picha ya pamoja ikiongozwa na
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndegulile wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali leo jijini Dar es salaam
……………
Na WAMJW-DAR ES SALAAM.
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeitaka
Mamlaka ya Maabara
ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuchukua hatua ya kupima maji yanayotiririka
mitaani kutoka viwandani kubaini kama yana kemikali ambazo zinaathiri
wananchi au hazina madhara yoyote.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa
Afy, Maendeleo ys Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile
wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya
Mkemia Mkuu wa Serikali leo jijini Dar es salaam.
“Bodi hii ninayoizindua leo
inatakiwa kuhakikisha majibu ya watu wanaokuja kuleta vipimo vyao
yatoke mapema na haraka iwezekanavyo ili kupunguza msongamano wa wateja
wenu” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa
Mamlaka hiyo inatakiwa kushirikiana na kufanya mazungumzo na Taasisi ya
Chakula na Dawa TFDA na TBS ili kutoingiliana katika majukumu kwani
kuna kuna kipengele cha majukumu yao kinafanana katika kusimamia ubora
wa chakula.
Aidha Dkt. Ndugulile ameitaka
Mamlaka hiyo kuisimamia kikamilifu sheria ya uchafuzi wa Mazingira ili
kuepusha wananchi na magonjwa ya kuambukiza na yasioambukiza.
Kwa upande wake Mkemia Mkuu wa
Serikali ambaye pia ni Katibu wa Bodi hiyo Dkt. Fidelis Mafumiko amesema
kuwa wanaiomba Serikali kutatua changamoto ya upungufu wa mitambo ya
kufanyia kazi katika mamlaka hiyo.
Aidha Dkt. Mafumiko amesema kuwa
Bodi hiyo iliyozinduliwa leo ipo tayari kufanya kazi kwa manufaa ya
Watanzania japo mamlka hiyo ina upungufu wa Watumishi kutoka watumishi
400 mpaka kufikia watumishi 220.
Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya
Mkemia Mkuu wa Serikali imezinduliwa leo ikiwa na Wajumbe saba ambao ni
Mwenyrkiti wa bodi hiyo Prof. Esther Hellen, Katibu Dkt. Fidelis
Mafumiko, Dkt. Eliud Eliakimu, Dkt. Samwel Gwamaka, Dcp. Hussein
Laiser, Bi. Irene Leisure na Bw. Pius Mponzi
No comments :
Post a Comment