![]() |
| Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo. |
![]() |
| Watendaji wa MGODI wa Dhahabu wa Geita (GGM) na Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) wakijadili jambo mara baada ya kumaliza mkuatano wa waandishi wa habari mapema leo. |
![]() |
||||||||
|
Dar es Salaam: Mgodi
wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya kuthibiti UKIMWI
Tanzania (TACAIDS) inatarajia kuzindua zoezi la upandaji wa mlima
Kilimanjaro (Kilimanjaro Challenge 2018), na kuendesha harambee ya
kuchangisha fedha kwa mwaka 2018 kwa ajili ya afua za UKIMWI nchini.
Shughuli hii inatarajiwa kufanyika tarehe 4 Mei 2018 mwaka huu katika
Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambapo atafanya zozezi la
ugawaji wa fedha zilizokusanywa mwaka mwaka jana 2017 zilizopatikana
baada ya wadau mbalimbali kupanda na kuendesha baiskeli kwa kuzunguzuka
Mlima Kilimanjaro .
Kilimanjaro
Challenge against HIV & AIDS ni mfuko unachangia juhudi za serikali
katika mapambano dhidi ya UKIMWI na kutoa elimu kwa jamii kuhusu
maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU).
Kilimanjaro
Challenge ni mfuko muhimu unaoshirikiana na taasisi za nje na ndani ya
nchi katika kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI kwa jamii ya
Kitanzania na Dunia kwa ujumla ili kuwapa matumaini ya kuhakikisha jamii
inabaki bila kuathiriwa na VVU/UKIMWI katika miaka ijayo.
Mfuko
huo pia unalenga kuisaidia Serikali kukabiliana na VVU//UKIMWI sambamba
na kutoa nafasi kwa watalii wa ndani na nje kuupanda mlima Kilimanjaro.
Takwimu
zilizotolewa na Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), zimeonesha
kupungua kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka asilimia 5.1 %
mwaka 2011/ 2012 hadi asilimia 4.7% mwaka 2016/17.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt. Leonard Maboko anasema, “
Mwaka wa 2016, inakadiriwa kuwa watu milioni 1.5 nchini wanaoishi na
VVU na UKIMWI hadi sasa watu 225 wanapata maambukizi ya virusi vya
UKIMWI kwa siku. Ugonjwa huu umewaathiri zaidi vijana na watoto yatima
zaidi. Tunahitaji kubadilisha hali hii. Lengo la kukusanya fedha ni
kuweza kusaidia serikali ya Tanzania katika jitihada zake kufikia sifuri
tatu. Sifuri katika maambukizi mapya, sifuri ya unyanyapaa, sifuri
katika vifo vitokanavyo na UKIMWI. TACAIDS kwa kushirikiana na Mgodi wa
Dhahabu wa Geita (GGM) na wadau wengine kwa kupitia mpango huu wa Kili
Challenge tunapenda kutoa mchango na ushirikiano wetu kwa Taifa ili
kutunisha mfuko utakaowezesha kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huu.
Tuna matumaini ya kujenga timu imara yenye hamasa ya kupambana na janga
hili. Tunatoa wito kwa makampuni na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya
nchi, wajitokeze ili tusaidiaane kutunisha mfuko wa Kili Challenge na
mwishowe kufikia malengo yetu ya kuhakikisha tunakuwa na kizazi kisicho
na maambukizi ya VVU/ UKIMWI,” alisema Dkt. Leonard Maboko.
“Watoto watakaoshiriki katika zoezi la Kilimanjaro Challenge mwaka huu ni wa kiume na wa
kike wenye umri kuanzia miaka 13. Watoto hao yatima kutokana na tatizo
la VVU/ UKIMWI wamesaidiwa na Kituo cha kulea watoto yatima cha Moyo wa
Huruma Orphanage Center kilichopo Geita.
Changamoto
kubwa inayotokana na janga hili ni pamoja na maelfu ya watoto yatima
wanaohitaji misaada baada ya wazazi wao kufariki, wajane wasiokuwa na
kipato, pamoja na wazee wanaolazimika kuwalea wajukuu walioachwa na
watoto wao ambao walifariki kutokana kwa ugonjwa huo.





No comments :
Post a Comment