Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimsalimia Mhifadhi
Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Dkt. Fredy Manongi
muda mfupi kabla ya kuanza kwa mashindano hayo. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
Waziri Kigwangalla akiwa tayari kuzindua mashindano hayo katika umbali wa kilomita 21.
Washiriki
wa mbio hizo kutoka Tanzania na Kenya wakitimua mbio kuanza mashindano
hayo ya Ngorongoro Marathon 2018 umbali wa Kilomita 21 mjini Karatu
mkoani Arusha. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishiriki mashindano
ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 na wanariadha wengine mjini Karatu
mkoani Arusha jana ambapo alimaliza mbio hizo kwa kukimbia kilomita 21.
Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha
utalii wa ndani.
Baadhi ya watalii nao walitumia fursa hiyo kusaka medali.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishiriki mashindano
ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 na wanariadha wengine mjini Karatu
mkoani Arusha jana ambapo alimaliza mbio hizo kwa kukimbia kilomita 21.
Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha
utalii wa ndani.
Baadhi ya washiriki wa mashindano hayo wakiwa katika harakati za kusaka medali.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishiriki mashindano
ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 na wanariadha wengine mjini Karatu
mkoani Arusha jana ambapo alimaliza mbio hizo kwa kukimbia kilomita 21.
Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha
utalii wa ndani.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akihitimisha mbio za
kilomita 21 za mashindano ya Ngorongoro Marathon 2018 yaliyofanyika
katika mji wa Karatu mkoani Arusha jana. Kaulimbiu ya mashindano hayo na
kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
Haikuwa kazi rahisi, washiriki wengine walilazimika kuvua viatu na kuvaa kandambili ili kurahisiha kazi yao ya kutafuta medali.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akionesha medali
aliyopewa pamoja na washiriki wengine wa mashindano ya mbio za
Ngorongoro Marathon 2018 yaliyofanyika mjini Karatu mkoani Arusha jana
ambapo alimaliza mbio hizo kwa kukimbia kilomita 21. Kaulimbiu ya
mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki nchini Tanzania, Filbert Bayi akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Rais
wa Chama cha Riadha Tanzania, Anthony Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu akitoa salamu zake katika hagla hiyo ambapo ameipongeza
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kufadhili mashindano hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mfaume Taka akizungumza na wananchi muda mfupi baada ya kumalizika kwa mbio hizo mjini Karatu.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza katika
mkutano wa hadhara wa kuhitimisha mashindano hayo mjini Karatu.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi cheti cha
shukurani Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro,
Dkt. Fredy Manongi kwa kufanikisha mashindano ya mbio za Ngorongoro
Marathon 2018 zilizofanyika katika mji wa Karatu mkoani Arusha jana.
Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha
utalii wa ndani.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi milioni moja
mshindi wa kwanza wa kilomita 21 kwa wanawake, Monica Chemko kutoka
Kenya katika mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018
zilizofanyika katika mji wa Karatu, wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha
jana. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na
kuhamasisha utalii wa ndani.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi milioni moja
mshindi wa kwanza wa kilomita 21 kwa wananume, Joseph Patha kutoka
Kenya katika mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018
zilizofanyika katika mji wa Karatu, wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha
jana. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na
kuhamasisha utalii wa ndani.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya
pamoja na baadhi ya washiriki wengine wa mashindano ya mbio za
Ngorongoro Marathon 2018 yaliyifanyika mjini Karatu mkoani Arusha jana
ambapo alimaliza mbio hizo kwa kukimbia kilomita 21.
Na Hamza Temba-Ngorongoro, Arusha
.....................................................................................
Mashindano
ya Olimpiki yatakayofanyika nchini Japan mwaka 2020 yatatumika kunadi
vivutio vya utalii vya Tanzania kupitia timu ya Taifa ya riadha na banda
la maonesho ya
utalii.
utalii.
Hayo
yameelezwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla
wakati akizungumza na wananchi muda mfupi baada ya kukamilika kwa
mashindano ya riadha ya Ngorongoro Marathon 2018 katika mji wa Karatu,
wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha jana.
Dkt.
Kigwangalla alitoa kauli hiyo wakati akijibu ombi la Rais wa Chama cha
Riadha Tanzania, Anthony Mtaka ambaye aliiomba wizara yake kupitia
Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kusaidia maandalizi ya timu ya
Taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano hayo.
Mtaka
pia aliomba Mamlaka hiyo itumie timu ya Taifa ya riadha Tanzania kama
mabalozi wao wa kutangaza vivutio vya utalii vya hifadhi hiyo ya
Ngorongoro ndani na nje ya nchi.
Akijibu
maombi hayo, Dk. Kigwangalla alisema kitaundwa kikosi kazi cha pamoja
kati ya wizara yake kupitia taasisi zake hususan Mamlaka ya Hifadhi ya
Eneo la Ngorongoro na Chama cha Riadha Tanzania ili kuainisha mahitaji
ya mashindano hayo na kuweka makubaliano yatakayonufaisha pande zote.
"Kama
tunaweza kupata jukwaa la nchi zaidi ya 50 au 100 kwa kufadhili
wanariadha 200 kwenda kushiriki, manake hilo jukwaa linatulipa, kwa
sababu tunawekeza kidogo tunaonekana kwa kiasi kikubwa.
"Mwaka
2020 kwenye Olimpiki lazima tuwekeze, na sisi Wizara ya Maliasili na
Utalii kupitia taasisi zetu tutapenda tuunde kikosi kazi cha pamoja ili
tuangalie gharama zinazohusika, maandalizi yanayohitajika ili na sisi
kama Wizara kupitia taasisi zetu kama Ngorongoro tuweze kuona nini
mchango wetu, lakini sisi tutataka tujue faida yetu hasa itakuwa ni
nini" alisema Dk. Kigwangalla.
Alisema
mashindano hayo yatatoa fursa pana kwa Taifa kutangaza vivutio vyake
mbali na juhudi zinazofanywa hivi sasa kupitia maonesho ya kimataifa.
"Kupitia mashindano hayo tutapeleka pia maombi kwenye ofisi ya balozi
wetu nchini Japan ili tupewe banda la kunadi vivutio vyetu vya utalii"
alisema.
Dk.
Kigwangalla pia aliitaka Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro
kukubali ombi la Chama cha Riadha Tanzania la kuanzisha kituo cha
mafunzo ya riadha mjini Karatu ili kuimarisha mchezo huo na timu ya
riadha Tanzania sambamba na kutumia kituo hicho kama fursa ya kutangaza
utalii wa hifadhi hiyo.
Alisema
kituo hicho pia kijengwe sanamu za wanariadha mashuhuri waliowahi
kuiletea sifa Tanzania na kuweka rekodi mbalimbali ili kutoa motisha kwa
wanariadha wengine wanaochipukia.
Alisema
mbali na kuanzisha kituo hicho, timu hiyo ya Riadha Tanzania inaweza
pia kupewa jina la Ngorongoro ili kuitangaza hifadhi hiyo yenye vivutio
vya kipekee duniani ambavyo vimeifanya itambulike kama sehemu ya urithi
wa dunia.
Mashindano
ya Ngorongoro Marathon kwa mwaka huu 2018 yamehusisha washikiri kutoka
Tanzania na Kenya ambapo washindi wa kwanza wa mbio hizo za kilomita 21
upande wanaume na wanawake wametoka nchini Kenya. Kaulimbiu ya
mashindano hayo imelenga kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa
ndani.
No comments :
Post a Comment