Diwani wa Kata ya Nyamagana Jijini
Mwanza ambaye pia ni Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji hilo Mhe. Bhiku
Kotecha (wa pili kushoto-mbele) akiwa na baadhi ya Madiwani na Wataalam
wa Halmashauri hiyo walipotembelea Dampo la kisasa la kuhifadhia
takataka lililopo eneo la Chidaya Jijini Dodoma jana. Mbele kushoto ni
Mhandisi wa Mazingira wa Jiji la Dodoma Barnabas Faida na kulia ni Afisa
Habari wa Jiji la Mwanza Martin Sawema.
Muonekano wa sehemu ya Dampo la kisasa la Chidaya Jijini Dodoma ambayo bado haijaanza kutumika.
Mhandisi wa Mazingira wa Jiji la Dodoma
Barnabas Faida na (kuhoto) akitoa maelezo kuhusu mradi wa Dampo la
kisasa la Chidaya kwa Madiwani na Wataalam wa Jiji la Mwanza
waliotembelea eneo hilo jana Aprili 27, 2018 kwa lengo la kujifunza.
Mhandisi wa Mazingira wa Jiji la Dodoma
Barnabas Faida na (kuhoto) akifuatilia maswali kuhusu mradi wa Dampo
la kisasa la Chidaya kutoka kwa Madiwani na Wataalam wa Jiji la Mwanza
waliotembelea eneo hilo jana Aprili 27, 2018 kwa lengo la kujifunza.
Operesheni za kuhifadhi takataka zikiendelea katika Dampo la kisasa la Chidaya Jijini Dodoma.
PICHA: RAMADHANI JUM-DCC
…………….
Na Ramadhani Juma,
Ofisi ya Mkurugenzi-DCC
MADIWANI wa Halmashauri ya Jiji la
Mwanza wameingia kwenye historia ya kuwa wageni wa kwanza kufanya ziara
ya kubadilishana uzoefu katika Halmashauri ya Jiji jipya la Dodoma mara
baada ya iliyokuwa Manispaa ya Dodoma kupandishwa hadhi na Rais wa
Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. John Magufuli wakati wa Sherehe za
miaka 54 ya Muungano Aprili 26, mwaka huu zilizofanyika katika uwanja ya
Jamhuri Jijini humo.
Madiwani hao wa jiji la Mwanza
wakiongozwa na Naibu Meya Mhe. Bhiku Kotecha ambaye ni Diwani wa Kata ya
Nyamagana, walitembelea Halmashauri ya Jiji la Dodoma jana Aprili 27,
2018 ikiwa ni siku moja tangu iliyokuwa Manispaa ya Dodoma kupewa hadhi
ya Jiji.
Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni
kubadilishana uzoefu hususan katika suala la Usafi wa Mazingira, ambapo
walitembelea Dampo la kisasa la kuhifadhia takataka kwa njia ya
kuzifukia (Sanitary Land Fill) lililopo eneo la Chidaya Kata ya
Matumbulu nje kidogo ya Jiji la Dodoma.
Wakiwa katika eneo la Dampo,
walipata maelezo ya kina juu ya mradi huo kutoka kwa Mhandisi wa
Mazingira wa Jiji la Dodoma Barnabas Faida, ambaye aliwaeleza kuwa,
mradi huo umetekelezwa kwa awamu kuanzia mwaka 2011 kwa Fedha za
Serikali Kuu ikiwa ni mkopo wa Benki ya Duniani kupitia mradi wa
kuimarisha Majiji ya Kimkakati (TSCP) na kwamba hadi kukamilika kwake
umegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 7.1, huku ukiwa tayari umeanza
kufanya kazi.
No comments :
Post a Comment