Tuesday, March 20, 2018

WENYE AMANA BENKI ZINAZOFILISIWA KUANZA KULIPWA MACHI 28,WADAI, WADAIWA WAPEWA NOTISI

Bank of Tanzania.
Benki kuu ya Tanzania 
Bodi ya Bima ya Amana (DIB) imetangaza ya kuwa kuanzia tarehe 28 Machi, 2018 itaanza kuwalipa fidia ya bima ya amana waliokuwa wateja wa benki tano ambazo zilitangazwa kufutiwa leseni za kufanya shughuli za kibenki tarehe 4 Januari mwaka huu.
Aidha, Bodi hiyo ambayo imepewa mamlaka na Benki Kuu ya Tanzania kuwa mfilisi wa taasisi hizo, imewataka wadaiwa na wadai wa taasisi hizo kujitokeza kuwasilisha vithibitisho vya madai yao ifikapo tarehe 17 Aprili, 2018.
Wenye amana watakaonufaika na malipo hayo ya fidia ya bima ya amana ni waliokuwa wateja wa Njombe Community Bank Ltd, Meru Community Bank, Covenant Bank for Women in Tanzania Ltd, Efatha Bank Ltd na Kagera Farmers’ Cooperative Bank Ltd, ambazo ziko katika ufilisi ambao watatakiwa kutimiza masharti kadhaa ili kupata malipo yao.
Masharti yaliyotajwa ni pamoja na kutambua mahali na muda wa malipo, ukomo wa malipo ya fidia, madai kwa amana zinazozidi shilingi 1,500,000, na kuwa na vitambulisho stahiki.
NB: Taarifa zaidi zinapatikana katika mtandao wa Benki Kuu: http:/www.bot.go.tzhttps:

No comments :

Post a Comment