Watendaji wa Wizara ya Nishati na
Taasisi zake wakimsikiliza waziri wa nishati Dkt. Medard Kalemani(
hayupo pichani) akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wanaotekeleza
mradi wa REA III uliofanyika katika ukumbi wa hazina Mkoani Dodoma.
wakisikiliza
Washiriki wa mkutano wa wadau
wanaotekeleza mradi wa REA III wakitoa maoni yao wakati wa mkutano huo
uliofanyika katika ukumbi wa hazina Mkoani Dodoma.
Watendaji wa Wizara ya Nishati na
Taasisi zake wakimsikiliza waziri wa nishati Dkt. Medard Kalemani(
hayupo pichani) akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wanaotekeleza
mradi wa REA III uliofanyika katika ukumbi wa hazina Mkoani Dodoma.
wakisikiliza
……………….
Na Zuena Msuya, Dodoma
Waziri wa Nishati Dkt. Medard
Kalemani amewateua Wahandisi Saba(7) kutoka Wizara ya Nishati
watakaoshirikiana na wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa REA III katika
kila Kanda ili kuboresha na kurahisisha utekelezaji wa Mradi huo kwa
ufanisi.
Dkt. Kalemani alifanya uteuzi huo
baada ya kufanya mkutano na Wadau mbalimbali wanaotekeleza Mradi wa REA
III wakiwemo, Wakandarasi, Wawekezaji wenye Viwanda vya
kutengeneza
miundombinu ya umeme kama vile Trasfoma, Mita, pamoja na nyaya za umeme ,
Mameneja wa Kanda, na Wahandisi wanaosimamia Mradi ya REA III nchi
nzima.
Mkutano huo ulifanyika katika
ukumbi wa Mikutano wa Hazina ulipo Makao Makuu ya Nchi Dodoma, ambapo
pamoja na mambo mengine ulilenga kujadili hatua zilizofikiwa katika
utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu pamoja na
changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa Mradi huo.
Dkt.Kalenani alisema Wahandisi
walioteuliwa watashirikiana na Wakandarasi wa REA III kutafanya kazi
mbalimbali pamoja na kuwa na mpango kazi wa kila wiki wa kila Mkandarasi
katika eneo husika ili kusisimamia kwa ukaribu utekelezaji wake.
Pia watarahisisha mawasiliano
yamoja kwa moja kutoka kwa wakandarasi hao na Wizara ya Nishati ili
kufahamu hatua waliofikia na changamoto watakazokuwa wakikabiliana nazo
kwa Lengo la kuzitafutia ufumbuzi wa haraka.
Awali akizungumza katika mkutano
huo Dkt.Kalemani aliwataka wakandarasi hao kutumia busara na uzalendo
zaidi katika kuwaunganisha Wananchi na Huduma ya Umeme Vijiji kupitia
Mradi wa REA III.
Alifafanua kuwa mbali na kuwepo
kwa mikataba inayawaongoza wakandarasi hao kutekeleza majukumu yao,
lakini Kuna maeneo ambayo wanapaswa kuyafikia pasipo kuangalia
makubaliano ya mkataba.
” Nawasihisi Sana wakandarasi
mtumie burasa na uzalendo kuunganisha Wananchi kwa mfano utakuta Kijiji
kina Shule au Zahanati lakini hakuna umeme ila kimepitiwa na mradi wa
umeme lakini kijiji hicho hakipo kwenye orodha ya vile vijiji mlivopewa
katika mkataba, nawasihi sana kwa hili,tumieni busara, najua
inawezekana kuunganisha ili Watanzania wenzetu wapate huduma Bora za
afya au watoto wetu wapate mazingira mazuri ya kujisomea”, alisema Dkt.
Kalemani
Aidha aliwataka Wakandarasi hao
kuendelea kutumia bidhaa za ndani katika kutekeleza Mradi huo pia
kununua bidhaa kutoka viwanda tofauti hapa nchini ili kuweka ushindani
wa kibiashara pamoja na bei.
Kwa upande wa wenye viwanda , Dkt.
Kalemani, aliwataka kuzalisha bidhaa zenye ubora na zenye viwango
vinavyotakiwa ili kuendelea kukuza soko la ndani na nje pia kuuza bidhaa
hizo kwa Bei nafuu zaidi.
Hata hivyo aliwaahidi wakandarasi
hao kuwa kwa sasa Serikali itaharakisha ulipaji wa madeni wanayoidai
tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Kwa upande wa TANESCO na REA, Dkt.
Kalemani aliwataka kutimiza wajibu wao na kuacha kufanya kazi kwa
mazoea kwani bado wananchi wengi wanahitaji kuunganishwa na huduma ya
umeme hivyo waongeze juhudi na kufanya kazi kwa kuzingatia weledi.
Aliwataja wa Wahandisi walioteuliwa kusimamia Mradi wa REA III kuwa Ni
Mhandisi Salum Inegeja
atakayesimamia Kanda ya Ziwa, Mhandisi John Kitonga Kanda ya Nyanda za
Juu, Mhandisi Juma Mkobya Kanda ya Magharibi, na Mhandisi Ahmed Chinemba
Kanda ya Kati.
Wengine ni Mhandisi Samuel Mgweno
Kanda ya Kaskazini,Mhandisi Christopher Bitesigirwe Kanda ya Pwani
pamoja na Mhandisi Styden Rwebangira Kanda ya Kusini.
No comments :
Post a Comment