Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora amewataka wafanyabiashara nchini
kuhamasika kujiunga na mtandao wa mitaji ya ubia ili kuimarisha vitega
uchumi vyao na pia kusaidia kuanzisha viwanda hapa nchini.
Profesa Kamuzora alisema
hayo wakati akizindua Mtandao wa Mitaji ya Ubia Tanzania – Tanzania
Venture Capital Network jijini Dar es salaam jana.
Aidha Katibu Mkuu huyo
amesema uzinduzi wa mtandao huo umefanyika wakati mwafaka ambapo
serikali ya awamu ya tano ipo katika mikakati ya kuigeuza Tanzania kuwa
nchi ya viwanda,
Aliwataka wananchi kuacha
uoga katika ushiriki wa kuwawezesha kuwepo kwa mitaji ya kutosha kwa
ajili ya uimarishaji wa uwekezaji nchini Tanzania.
Alisema serikali kwa sasa
inafanya kila linalowezekana kuhakikisha mazingira ya biashara na
uwekezaji yanakuwa bora, ndio maana wameanzisha mchakato wa kutengeneza
sera ya maendeleo ya viwanda hasa katika sekta binafsi.
Alisema ni vyema wenye
viwanda na wananchi wengine kushiriki katika mchakato huo ili
kufanikisha nia ya kuipeleka Tanzania katika nchi ya viwanda. Alisema
kwa kuwa na sera sheria nyingi zitabadilika na hivyo kupunguza urasimu
na pia vikwazo vya kuwezesha kazi katika masuala ya viwanda na biashara.
Pia alitaka wamiliki wa Ubia huo kushirikiana na Costech katika kuhakikisha kwamba viwanda vinaanzishwa na kuendelezwa.
Alitaka kuwepo na elimu ya fedha na mitaji ili wananchi waweze kuthubutu na kufanikisha mitaji.
Mapema Mwenyekiti wa
Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr. Reginald Mengi amewataka
wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa uwazi, kwa kuzingatia sheria za
nchi, na kuwa tayari kujifunza maarifa mapya kila fursa inapojitokeza.
Akisitikishwa na
mahudhurio duni ya wafanyabiashara katika hafla hiyo alisema kutofahamu
undani wa soko la mitaji na fursa zake kunatokana na kutokuwa wazi na
kufanya biashara kwa kufuata kanuni.
Akizungumzia kuhusu madai
ya kuwapo kwa hali kuwa ngumu nchini Dr. Mengi pia amewataka Watanzania
kuichukulia hali hiyo kama fursa ya kubuni biashara itakayowawezesha
kupata faida kubwa.
Akiutambulisha Mtandao wa
Tanzania Venture Capital kwa wadau, Muasisi wake Bw. Salum Awadh
amesema Mtandao huo ni fursa kwa wawekezaji nchini kujipatia mitaji ya
kuanzisha ama kuendeleza biashara zao kwa ubia kwa masharti rahisi.
Alisema kwamba wakati
umefika kwa Tanzania kusonga mbele kutumia fursa zilizopo duniani za
mitaji na kusema jirani zetu wa Kenya wamesonga mbele katika hilo.
Alisema kwamba kutokana na
kutojua umuhimu na ushiriki katika mitaji yenye ubia, wananchi wengi
wanakimbilia katika mabenki ya biashara ambako pia wanapambana na
vikwazo vingine.
Alisema kwa kuwa na
kampuni ya mitaji inayoweza kutafuta pia mtaji inayomilikiwa na wananchi
wenyewe kupitia mitaji yao kutawezesha kuwapo na uimara wa viwanda na
kuongeza idadi zake kwa kuwa mfumo wa fedha wa mitaji ni tofauti na
kwenda benki.
Tanzania kwa sasa ina
zaidi ya mabenki 50 ambayo yanajishughulisha na mambo mbalimbali
yanayogusa biashara na hifadhi ya kawiada.
Alisema mazingira ya sasa
yanahitaji mfumo mwingine wa ziada kusaidia upatikanaji wa mitaji nje ya
mabenki na kuzinduliwa kwa mtandao wa ubia wa mitaji kutasaidia kuziba
pengo lililopo.
Kwa sasa Tanzania kwa
rekodi zilizopo inapata asilimia 17 ya mitaji ya ubia ya dola bilioni
2.4 iliyopo duniani huku Kenya ikiwa na nfasi nzuri zaidi.
Hafla hiyo imehudhuriwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta Binafsi nchini-TPSF Bw. Godfrey
Simbeye, baadhi ya viongozi wa taasisi za serikali na wafanyabiashara
mbalimbali.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini Bw. Godfrey Simbeye
(kushoto) akifafanua jambo kabla ya kuanza kwa uzinduzi wa Mtandao wa
Mitaji ya Ubia Tanzania – Tanzania Venture
Capital Network uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam, Wanaomsikiliza ni Muasisi wa Mtandao wa Tanzania Venture
Capital, Bw. Salum Awadh (wa pili kushoto aliyesimama), Mwenyekiti wa
Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi (wa pili kulia)
pamoja Mkurugenzi wa Uwekezaji na Maendeleo ya Viwanda –TPSF, Edward
Furaha (kulia).
Muasisi wa Mtandao wa
Tanzania Venture Capital, Bw. Salum Awadh akitoa maelezo kuhusu Mtandao
wa Tanzania Venture Capital kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu Prof. Faustine Kamuzora (kushoto) kabla ya kuelekea kwenye hafla
ya uzinduzi wa mtandao huo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta
Binafsi nchini Bw. Godfrey Simbeye (wa pili kushoto) pamoja na
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi
(kulia).
Muasisi
wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital, Bw. Salum Awadh akitoa neno la
ukaribisho na kutambulisha mtandao huo ambapo amesema ni fursa kwa
wawekezaji nchini kujipatia mitaji ya kuanzisha ama kuendeleza biashara
zao kwa ubia kwa masharti rahisi wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa
mtandao huo ilyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya
Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi akitoa neno la ufunguzi
kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
Prof. Faustine Kamuzora kutoa hotuba ya uzinduzi wa Mtandao wa Tanzania
Venture Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam.
Mgeni
rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora akitoa
hotuba ya uzinduzi rasmi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital ambapo
amesema umefanyika wakati mwafaka ambapo serikali ya awamu ya tano ipo
katika mikakati ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda katika hafla
fupi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Uwekezaji na Maendeleo ya Viwanda –TPSF, Bw. Edward Furaha na
Aliyekuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Abdullah Mwinyi
wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye hafla ya
uzinduzi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital uliofanyika katika
Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Pichani
juu na chini ni sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa
Mtandao wa Tanzania Venture Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr. Reginald Mengi
akisalimiana na kubadilishana mawazo na wageni waalikwa waliohudhuria
hafla ya uzinduzi wa wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital uliofanyika
katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya
Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr. Reginald Mengi akibadilisha na mawazo na
Afisa Mtendaji Mkuu wa DOB Equity, Brigit van Dijk-van de Reijt wakati
wa hafla ya uzinduzi wa wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital
uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wengine ni
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora
(wa tatu kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta
Binafsi nchini-TPSF Bw. Godfrey Simbeye (kushoto).
Tanzania
Venture Capital Network-TVCN katika picha ya pamoja na mdau
aliyewezesha kufanyika kwa uzinduzi wa Mtandao wa Tanzania Venture
Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
No comments :
Post a Comment