Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akizungumza na Wajumbe wa kamati
ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama wakati wa kupokea
na kujadili taarifa ya Wizara ya ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa
iliyofanyika Wilayani kilwa Mkoani Lindi. kushoto ni Mwenyekiti wa
kamati hiyo, Mhe. Mussa Zungu, Makamu Mwenyekiti Mhe. Salum Rehani (wa
pili kushoto) na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa, Dkt. Florence Turuka
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya
Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama, Mhe. Mussa Zungu akizungumza
na Wajumbe wa kamati hiyo, watendaji wakuu toka wizarani, ngome, kamandi
ya wanamaji na halmashauri ya wilaya ya kilwa wakati kupokea na
kujadili taarifa ya Wizara ya ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa
iliyofanyika Wilayani kilwa Mkoani Lindi. Kulia ni Waziri wa Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi, kushoto ni Makamu
Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Salum Rehani na wa pili kushoto ni Mkuu
wa kamandi ya Wanamaji, Meja Jenerali Richard Mtayoba
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya
Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama wakikagua Mradi kuhusu Tathmini
na ulipaji wa fidia ya Ardhi, kilwa Navy Military Base katika tukio
lililofanyika wilayani kilwa Mkoani Lindi.
Mkuu wa kamandi ya Wanamaji, Meja
Jenerali Richard Mtayoba akiwapa maelezo Wajumbe wa kamati ya kudumu ya
Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama wakati alipoenda kukagua Mradi
kuhusu Tathmini na ulipaji wa fidia ya Ardhi, kilwa Navy Military Base
katika tukio lililofanyika wilayani kilwa Mkoani Lindi.
Mkuu wa kitengo cha usimamizi na
Maendeleo ya Miliki kutoka Wizara ya ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa,
Ndg. Sebastian Bebwa akiwapa maelezo mafupi Wajumbe wa kamati ya kudumu
ya Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama kabla ya kwenda kukagua
Mradi kuhusu Tathmini na ulipaji wa fidia ya Ardhi, kilwa Navy Military
Base katika tukio lililofanyika wilayani kilwa Mkoani Lindi.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE
No comments :
Post a Comment