Pichani wahamiaji haramu kutoka
nchini Ethiopia ambao wamekamatwa na jeshi la polisi Mkoani Pwani ,huko
porini Pingo shule ,wilaya ya kipolisi Chalinze
Kamanda wa polisi Mkoani Pwani, (ACP) Jonathan Shanna akizungumza kuhusiana na misako na doria zinazoendelea Mkoani humo.
Picha na Mwamvua Mwinyi
……………..
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
JESHI la polisi mkoani Pwani,
limewakamata wahamiaji haramu kumi raia wa nchi ya Ethiopia ,kwa kosa
la kuingia nchini bila kibali.
Jeshi hilo pia, limemtia nguvuni
mwanamke -Siwema Mgombale akiwa na risasi 23 zinazotumika kwenye silaha
aina ya shortgun, huko kijiji cha Manda Mazingara kata ya
Miono,tarafa
ya Mkange wilaya ya Bagamoyo.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani,
(ACP), Jonathan Shanna alisema, wahamiaji haramu hao wamekamatwa machi
26, wakiwa porini ,Pingo Shule ,wilaya ya kipolisi Chalinze na askari
waliokuwa doria kufuatia kupata taarifa kutoka kwa raia wema.
Akielezea matukio mbalimbali
yaliyotokea mkoani hapo, aliwataja waliokamatwa kuwa ni Tagen Alam (19),
Abraham Wolde (19) na Musama Kamal (16).
Wengine ni Abush Tamaskel (16),
Ayela Erapo (18) na Ngusie Kechine (18), Zarabel Faisa (16), Tsedhj
Yshgee (19), Teyey Ally (18) na Tuktigo Clemag (17).
Watuhumiwa wote hao watafikishwa idara ya uhamiaji kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Kamanda Shanna alielezea ,jeshi
hilo linaendelea na juhudi za kuwatafuta watu waliowasaidia kuingia
nchini bila kufuata utaratibu wa sheria.
Katika tukio jingine , mwanamke
aliyejulikana kwa jina la Felister Mtinga (30-36) amekutwa kitandani
akiwa amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni iitwayo
Moreto,iliyopo Chalinze.
Kamanda Shanna alisema kuwa, mwili
wa mwanamke huyo ulibainika machi 26 mwaka huu majira ya saa nne
asubuhi baada ya wahudumu kutomuona akitoka tangu alipoingia ndani machi
25 katika nyumba hiyo.
Alifafanua , mwili wa marehemu
umeshafanyiwa uchunguzi wa awali na kubaini kutokuwa na majeraha ya aina
yoyote hali inayosababisha kuondoa mashaka kuhusu kifo chake na
umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa ya Tumbi.
Katika tukio la kukutwa na silaha,
kamanda Shanna alibainisha wamekamata silaha mbalimbali katika misako
inayoendelea kufanyika mkoani hapo, ikiwemo SMG .R.6134, mapanga manne,
sime moja na risasi 23.
Alieleza, saa sita usiku machi
27,walimkamata mwamke aliyetambulika kwa jina la Siwema Mgombale akiwa
na risasi 23 zinazotumika kwenye short gun na Ramadhani Mdoe akiwa na
silaha aina ya SMG.R.6134 .
“Tunaendelea na misako kabambe
inayoongozwa na kikosi chao cha siri, tunafanya misako uvungu kwa
uvungu,giza kwa giza,pori kwa pori,tunashukuru inazidi kufanikiwa na ni
endelevu “alisisitiza kamanda huyo.
Kamanda Shanna aliwaomba wananchi
kushirikiana na jeshi la polisi kutoa taarifa za wale wachache ambao
wanawadhania ni wahalifu kwenye maeneo yao.
No comments :
Post a Comment