Mkurugenzi wa Taasisi ya Twaweza,
Aidan Eyakuze akiwasilisha ripoti ya utafiti wa taasisi hiyo kuhusiana
upatikanaji wa taarifa na uhuru wa habari mbele ya wadau mbalimbali wa
habari. Mkutano huo ulifanyika leo alhamisi Machi 29, 2018.
Baadhi ya wadau wa habari kutoka
taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa wakifuatilia mkutano
ulioandaliwa na taasisi ya Twaweza kuhusiana na hali ya upatikanaji wa
taarifa na dhana ya uhuru wa habari nchini. Mkutano huo ulifanyika leo
alhamisi Machi 29, 2018.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi akifuatilia mkutano uliondaliwa na taasisi
ya Twaweza kuhusiana na hali ya upatikanaji wa taarifa na dhana ya
uhuru wa habari nchini. Mkutano huo ulifanyika leo alhamisi Machi 29,
2018.
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe
akifuatilia mkutano uliondaliwa na taasisi ya Twaweza kuhusiana na hali
ya upatikanaji wa taarifa na dhana ya uhuru wa habari nchini. Mkutano
huo ulifanyika leo alhamisi Machi 29, 2018.
Baadhi ya wadau wa habari kutoka
taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa wakifuatilia mkutano
ulioandaliwa na taasisi ya Twaweza kuhusiana na hali ya upatikanaji wa
taarifa na dhana ya uhuru wa habari nchini. Mkutano huo ulifanyika leo
alhamisi Machi 29, 2018.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Vicensia Shule akizungumza na wadau mbalimbali wa habari wakati
wa mkutano ulioandaliwa na taasisi ya Twaweza kuhusiana na hali ya
upatikanaji wa taarifa na dhana ya uhuru wa habari nchini. Mkutano huo
ulifanyika leo alhamisi Machi 29, 2018.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na
wadau mbalimbali wa habari wakati wa mkutano ulioandaliwa na taasisi ya
Twaweza kuhusiana na hali ya upatikanaji wa taarifa na dhana ya uhuru
wa habari nchini. Mkutano huo ulifanyika leo alhamisi Machi 29, 2018.
(NA MPIGAPICHA WETU
……………….
Na Mwandishi Wetu,
MAELEZO
DAR ES SALAAM
SERIKALI imesema haijazuia
vyombo vya habari kukosoa utekelezaji wa sera, mikakati na programu zake
na badala yake imewataka kuzingatia miiko na maadili ya taaluma hiyo
yaliyoanishwa sheria za kimataifa.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar
es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa
Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati wa uzinduzi wa Awamu ya 25 ya
utafiti wa sauti ya wananchi iliyotolewa na taasisi ya Twaweza.
Dkt. Abbasi alisema kumepo na
mkanganyiko mkubwa kuhusu dhana ya uhuru wa habari, hatua
inayosababisha baadhi ya vyombo vya habari kuandika na kutangaza taarifa
mbalimbali ambazo zimekuwa zikikiuka misingi ya sheria za nchi.
“Vipo baadhi ya watu wamekuwa
wakifikiri dhana ya uhuru ni kusema chochote na kutumia lugha ya kejeli,
hivyo ripoti hii ya utafiti tumeweza kuwa na wataalamu mbalimbali
waliokuwa wakitoa mada na kujadili kwa kina misingi na miiko ya uhuru wa
habari” alisema Dkt. Abbasi.
Alisema kuwa dhana ya uhuru wa
habari ipo katika sheria mbalimbali za kimataifa iliyoanishwa katika
misingi ya haki na wajibu, na hivyo ni wajibu wa wadau mbalimbali
kuwawezesha wananchi na vyombo vya habari nchini kuweza kuelewa dhana
hiyo.
Alioongeza kuwa Serikali
imeendelea kuongeza wigo mpana wa uanzishaji wa vyombo vya habari nchini
ikiwemo kutoa idadi kubwa ya leseni za uanzishaji wa vituo vya redio
hususani katika maeneo ya vijijini, hatua inayolenga kuwawezesha
wananchi kuweza kupata taarifa mbalimbali za umma.
Kuhusu taarifa ya utafiti huo,
Dkt. Abbasi alisema Serikali itatumia taarifa ya ripoti ya utafiti huo
kupata mrejesho na kuainisha maeneo yote ili kuchambua hoja na kuweza
kuangalia maeneo yenye changamoto ili kuweza kuboresha mfumo wa utoaji
na upatikanaji wa taarifa za Serikali kwa wananchi.
Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alisema
Serikali tayari imetoa maelekezo kwa Maafisa Habari na Mawasiliano wa
Taasisi zote za umma nchini kuweka utaratibu wa kutoa taarifa zake kwa
umma kwa kuwa suala la utoaji wa taarifa si utashi na badala yake ni
utekelezaji wa matakwa ya sheria.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
Taasisi ya Twaweza, Aidan Eyakuze alisema katika utafiti huo uliohusisha
jumla ya watu 1500, ulionyesha kuwa wananchi wana imani na taarifa na
imani zinazotolewa na Viongozi Wakuu wa Serikali ikiwemo Rais ikifuatiwa
na Waziri Mkuu.
No comments :
Post a Comment