Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya
uandishi wa habari za tovuti kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya
Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga wakifuatilia mada
mbalimbali wakati wa mafunzo hayo yaliyofunguliwa jana Jumanne Machi 20,
2018 Mkoani Morogoro. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na
Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili
wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID)
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya
uandishi wa habari za tovuti kutoka katika Mikoa na Halmashauri
mbalimbali nchini wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo hayo
yaliyofunguliwa jana Jumanne Machi 20, 2018 Mkoani Morogoro. Mafunzo
hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya
Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la
Marekani (USAID).
Afisa Tehama kutoka Halmashauri ya
Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro, Alfred Chali akichangia hoja wakati
wa mafunzo ya uandishi wa habari za tovuti kutoka katika Halmashauri na
Mikoa ya Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga yaliyofunguliwa
jana Jumanne Machi 20, 2018. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na
Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia
ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Habari (MAELEZO), Rodney Thadeus akizungumza na Maafisa Habari na
Mawasiliano kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Morogoro, Manyara,
Dodoma, Kilimanjaro na Tanga yaliyofunguliwa jana jumanne Machi 20,
2018. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji
Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la
Misaada la Marekani (USAID).
Mwezeshaji na Afisa Habari kutoka
Ofisi ya Rais TAMISEMI, Nteghenjwa Hosseah akiwasilisha mada kuhusu
mtindo wa uandishi wa habari katika tovuti kutoka katika Halmashauri na
Mikoa ya Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga yaliyofunguliwa
jana Jumanne Machi 20, 2018. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na
Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia
ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
(NA MPIGAPICHA WETU
…………………
Na Mwandishi Wetu,
MAELEZO
MOROGORO
MAAFISA Habari na Mawasiliano
katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini wametakiwa kuacha
kufungia katika makabati na makabrasha taarifa chanya za utekelezaji wa
mikakati, miradi na programu mbalimbali za Serikali na badala yake
watangaze mafanikio hayo kwa umma.
Hayo yamesemwa jana (Jumanne Machi
20, 2018) Mkoani Morogoro na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari
(MAELEZO), Rodney Thadeus wakati wa ufunguzi wa mafunzo kuhusu mwongozo
wa uandishi wa habari za tovuti kupitia Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya
Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani
(USAID).
Thadeus alisema Serikali
inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika Mikoa na Halmashauri
mbalimbali nchini, hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano
katika maeneo hayo watangaze mafaniko hayo badala ya kusubiri maswali na
hoja mbalimbali za wananchi wakihoji katika kupata uelewa kuhusu miradi
hiyo.
“Maafisa Habari, msifungie taarifa
katika makabati yenu toeni taarifa kwa Umma, wananchi wanapenda
kufahamu nini kinafanywa na Serikali yao hivyo jukumu la Afisa Habari ni
kupiga picha kuandaa taarifa na wekeni vielelezo hivyo katika tovuti
zenu ili kujibu hoja za wananchi” alisema Thadeus.
Aidha, alisema ni wajibu wa
Maafisa Habari na Mawasiliano kuhakikisha kuwa wanaweza taarifa mpya
kila wakati ili kuhakikisha kuwa zinakidhi mahitaji ya msingi ya
wananchi ambao wamekuwa wakitumia muda mrefu kwa ajili ya kutafuta
huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali katika maeneo yao ya kazi.
Akifafanua zaidi alisema Maafisa
Habari na Mawasiliano katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini
ndiyo wataalamu wa masuala ya Mawasiliano katika maeneo yao ya kazi,
hivyo wana wajibu wa kutoa ushauri kwa viongozi wao wa kazi kwa ajili ya
kutoa ufafanuzi wa mara kwa mara kuhusu hoja mbalimbali zinazoulizwa na
kujitolea majibu kwa wakati.
Aliongeza kuwa matumizi ya tovuti
ndiyo njia ya haraka zaidi ya kurahisisha mfumo wa utoaji wa habari na
taarifa mbalimbali za Halmashaauri na Mikoa, hivyo ni wajibu wa Maafisa
Habari na Mawasiliano kuwa mabalozi ili kuhakikisha kunakuwepo na daraja
la mawasiliano baina ya Serikali na wananchi katika kupata suluhu ya
masuala mbalimbali ikiwemo migogoro inayotokea mara kwa mara.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Timu
ya Utawala Bora kutoka PS3, Dkt. Peter Kilima alisema uboreshaji wa
tovuti ni sehemu muhimu ya utekelezaji wa dhana halisi ya utawala bora
hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano katika Mikoa na
Halmashauri nchini kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa
zinazozingatia muda na mahitaji yaliyopo.
Aliongeza ni wajibu wa Maafisa
Habari na Mawasiliano kuzingatia mafunzo kuhusu mwongozo wa uandishi wa
habari katika tovuti za Serikali katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali
nchini kwa kuwa wananchi wana matarajio makubwa na Serikali yao katika
kuwapatia huduma mbalimbali.
No comments :
Post a Comment