Waziri
wa Mali Asili na Utalii mhe. Dkt. Hamis
Kigwangala (katikati) akiimba wimbo wa
mshikamano pamoja na Katibu Mkuu Wizara
ya Mali Asili na Utalii Meje Jenerali Gaudensi Milanzi pamoja na Viongozi wa
Shirikisho la Wafanyakazi.
Waziri
wa Mali Asili na Utalii mhe. Dkt. Hamis
Kigwangala akihutubia Wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa Kikao cha Baraza la
Wafanyakazi kilichofanyika mjini Dodoma.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mali Asili na Utalii Meje
Jenerali Gaudensi Milanzi akizungumza na
Wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi
kilichofanyika mjini Dodoma.
Sehemu
ya watumishi wa Wizara ya Mali Asili na
Utalii wakifuatilia hotuba Waziri wa
Mali Asili na Utalii mhe. Dkt. Hamis
Kigwangala ambaye alikuwa mgeni
rasmi wakati wa kikao cha Baraza la
Wafanyakazi wa Wizara hiyo leo mjini Dodoma.
Sehemu
ya Wakurugenzi wa Wizara ya Mali Asili na Utalii Wakiimba wimbo wa mshikamano
wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo leo mjini Dodoma.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mali Asili na Utalii Meje
Jenerali Gaudensi Milanzi akimpokea Waziri wa Mali Asili na Utalii Mhe. Dkt. Jumanne
Kigwangala mapema leo mjini Dodoma
ambapo alikuwa mgeni rasmi katika kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Wizara
hiyo.
FRANK MVUNGI- MAELEZO, DODOMA.
Tanzania
imefanikiwa kuongeza idadi ya watalii kutoka 1,284,279 mwaka 2016 hadi kufikia 1,327,143 mwaka 2017 hali iliyopelekea kuongezeka kwa mapato ya Serikali.
Akizungumza
wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mali Asili na Utalii
Dkt. Hamis Kigwangala amesema Wizara hiyo itaendelea kuvutia watalii zaidi ili
kukuza utalii na kuongeza pato la Taifa.
“Mapato
yanayotokana na utalii yameongezeka kutoka Dola za Kimarekani Bilioni 2.1 mwaka
2016 hadi Dola za Kimarekani Bilioni 2.2 mwaka 2017” Alisisitiza Kigwangala
Akifafanua
Dkt. Kigwangala amesema lengo la Serikali ni kuona mafanikio haya yanazidi
kuimarika, hivyo kila mtumishi katika Wizara hiyo lazima atimize wajibu wake ipasavyo.
Aliongeza kuwa ili kufanikisha majukumu ya Wizara
hiyo ipasavyo ni muhimu kuwa na bajeti ambayo itawezesha kushughulikia
changamoto za migogoro ya mipaka katika maeneo ya hifadhi, kufanya mapitio ya
Sera, Sheria na Kanuni mbalimbali, upungufu wa watumishi, uhaba wa vitendea
kazi, kutoa elimu ya maadili na kusimamia watumishi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja
Jenerali Gaudensi Milanzi amesema kuwa Wizara hiyo itazingatia ushauri
unaotolewa na watumishi wake ili kuongeza tija katika kutatua changamoto zinazojitokeza.
“Wizara itaendelea kupambana dhidi
ya ujangili, biashara haramu ya nyara na magogo na kuwachukulia hatua kali
watumishi wote watakaogundulika kukiuka maadili ya utumishi wa umma kwa
kushiriki katika vitendo hivyo “ Alisisitiza Meja Jenerali Milanzi
Wizara
kwa mwaka wa fedha 2017/2018 iliendelea na utaratibu wa kuendeleza watumishi
katika mafunzo ya aina mbalimbali kama ifuatavyo:-Jumla ya watumishi wanne (4)
wanahudhuria mafunzo ya muda mrefu nje na ndani. Aidha, mtumishi mmoja(1) yupo
nje ya nchi.
Watumishi
wengine kumi na moja (11) walihudhuria
mafunzo ya muda mfupi. Mafunzo haya yalihusu watumishi wa kada mbalimbali.
Jumla
ya watumishi saba (7) wamehudhuria mafunzo ya ujasiliamali unaohusiana na
maandalizi ya kustaafu. Aidha, Wizara bado inaendelea na utaratibu wa kuwaandaa
watumishi wote wanaokaribia kustaafu kuhakikisha wanapata mafunzo hayo.
Wizara
ya Mali Asili na Utalii imekuwa ikipambana na ujangili, biashara haramu ya
nyara, magogo na kuwachukulia hatua kali
za kinidhamu na kisheria kwa watumishi wote watakaogundulika kukiuka
maadili ya utumishi wa umma kwa kushiriki katika vitendo hivyo.
No comments :
Post a Comment